BANDA MEDIA BLOG

MAAFISA KAZI WATAKIWA WATAKIWA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

 

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwan Jakaya Kikwete amewataka Maaafisa Kazi Wafawidhi nchini kuongeza ubinifu katika usuluhishi wa migogoro mahala pa kazi wito alioutoa Morogoro wakati alipofungua kikao kazi 12 Septemba 2025.

Na. OWM-KVAU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amewaagiza Maafisa Kazi Wafawidhi nchini kuendeleza ubunifu katika utendaji wao wa kazi huku wakizingatia maadili ya utumishi wa umma.

 

Amewasisitiza kutoa huduma bora na kwa wakati hususani katika maeneo nyeti yanayohusisha usuluhishi wa migogoro ya kikazi na malalamiko ya wananchi mara yanapofikishwa kwenye ofisi zao.

 

Maafisa Kazi Wafawidhi toka mikoa  ya Tanzania Bara wakiwa kwenye kikao kazi  cha kuandaa mwongozo wa ukaguzi mahali pa kazi mjini Morogoro 12 Septemba 2025.

Waziri Ridhiwani alieleza hayo Septemba 12, 2025 mkoani Morogoro wakati wa Kikao kazi cha kuandaa mwongozo wa ukaguzi mahali pa kazi ili kujumuisha masuala ya wafanyakazi wa Nyumbani, Watu wenye Ulemavu na Utumikishwaji wa Mtoto.

 

Katika hatua nyingine, amewataka Maafisa hao kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa jamii kwa kushirikiana na wadau wa Utatu amba oni Serikali, vyama vya waajili ana vyama vya wafanyakazi katika kushughulikia changamoto za kikazi.

 Kikao hicho kiliwahusisha viongozi wa Idara ya Kazi, Msajili wa Vyama Vyama vya Wafanyakazi, pamoja na Maafisa Kazi Wafawidhi wa Mikoa yote Tanzania.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwan Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Kazi Wafawidhi mara baada ya kufungua kikao kazi 12 Septemba 2025 mjini Morogoro.

(Habari na Picha : OWM-KVAU)

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG