BANDA MEDIA BLOG

WANAWAKE NA SAMIA WAMPA KONGOLE RAIS SAMIA KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 66

 

Katibu wa Wanawake na Samia Mkoani Dodoma, Neema Ndashao akiwalisha Keki wanafunzi wa Shule ya Msingi Kaloleni jijini humo, wakati wa hafla ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Katibu wa Wanawake na Samia Mkoani Dodoma, Neema Ndashao akipanda mti katika Shule ya Msingi Kaloleni jijini humo, wakati wa hafla ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

NA JOHN ISRAEL, BANDA MEDIA DODOMA

WANAWAKE na Samia Mkoa wa Dodoma Januari 27,2026 wameungana na wanafunzi wa shule ya msingi kaloleni jijini humo Pamoja na  watanzania kwa ujumla kumtakia Heri ya Kuzaliwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyezaliwa mnamo mwaka 1960. Kwa kupanda miti ya matunda Pamoja na kukata keki ya Upendo

Akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika katika shule ya msingi Kaloleni jijini humo Katibu wa Wanawake hao Mkoa wa Dodoma, Neema Ndashao amesema wamepanda miche ya miti 30 ya matunda kwa lengo la kumuunga mkono Rais Samia kwa kutimiza miaka 66

Ndashao amesema, Rais Samia ndiye kinara wa mazira hapa nchini tangu akiwa makamu wa Rais, na kwamba amekuwa akisisitiza umuhimu wa kupanda miti na kutunza mazingira.

“tunamuunga mkono mama Samia kwa kupanda miti ili kulinda na kutunza mazingira, Pamoja na kukata keki ya upendo na wanafunzi tukisherekea pamoja naye siku yake ya kuzaliwa”, amesema

Nae Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Kaloleni, Jackison Jumbe ambapo Tukio hilo limefanyika amesema shule hiyo imetenga eneo la bustani ya matunda maalumu, na kwamba wataitunza miti hiyo ili itakapoonza kuzaa matunda yawafae wanafunzi

“tunashukuru kitendo cha wanawake na samia kuja kupanda miti shuleni kwetu, inasaidia kutunza mazingira ukizingatia rais katujengea majengo mapya, hivyo matunda yakianza yatawasaidia wanafunzi kupata mlo kamili”, amesema

kwa upande wake mwalimu Selina Nyagawa anayefundisha darasa la tatu akisimamia Idara ya Mazingira shuleni hapo, amesema kila mti utakabidhiwa mwanafunzi wa kuutunza hivyo hakuna utakaokufa ikizingatiwa kuna maji ya kutosha shuleni hapo

“tunampongeza Rais Samia kwa Siku yake ya Kuzaliwa, tutaitunza hii miti mpaka izae Matunda kwa ajili ya nafunzi, pia tumuahidi kufanya kazi kwa weredi na kuwapa Watoto matokeo tarajiwa”, amesema

wanafunzi  wamemshukuru Rais Samia na kumtakia Maisha marefu, huku wakimpongeza kwa kuihudumia shule hiyo kwa kuijengea miundombinu Pamoja na vyumba vya madarasa.

Ikumbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amitimiza jumla ya Miaka 66 tangu kuzaliwa kwake.









Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG