BANDA MEDIA BLOG

Kivu Kaskazini - Anguko la Viongozi wa M23 na Mchezo mpya wa Drone za Kivita

 


Jenerali Sultani Makenga ni miongoni mwa majina makubwa yanayohusishwa na harakati za waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Anatokea eneo la mashariki mwa nchi hiyo, ambayo kwa muda mrefu limekumbwa na migogoro ya kikabila na vita vya makundi yenye silaha.

Makenga alianza kuhusika na makundi ya waasi mapema, hasa yale yaliyojitambulisha kutetea maslahi ya Watutsi wa Kongo. Kabla ya kuibuka kwa M23, alikuwa sehemu ya kundi la waasi la Congrès National pour la Défense du Peuple (CNDP) lililoongozwa na Laurent Nkunda. CNDP lilidai kulinda jamii ya Watutsi dhidi ya vitisho kutoka makundi kama Forces Démocratiques de Libération du Rwanda (FDLR).
Mwaka 2012, Makenga aliteuliwa kuwa kamanda mkuu wa kijeshi wa M23, kundi lililoanzishwa na wanajeshi wa zamani wa CNDP waliodai kuwa serikali ya DRC haikutekeleza makubaliano ya amani ya tarehe 23 Machi 2009 — chanzo cha jina “M23”.
Chini ya uongozi wake, M23 iliteka mji wa Goma na miji mingine mikubwa masharikimwaDRC, tukio lililotikisa siasa za eneo hilo na kuvuta hisia za jumuiya ya kimataifa.
Ndani ya M23 kulizuka mgawanyiko kati ya Makenga na aliyekuwa kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo, Jean-Marie Runiga, aliyekuwa akihusishwa zaidi na Bosco Ntaganda. Mgogoro huo uliishia Makenga kushinda upande wa Ntaganda, ambaye baadaye alijisalimisha kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Kuporomoka na kurejea kwa M23
Mwaka 2013, M23 ilishindwa kijeshi na jeshi la DRC kwa msaada wa kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa (FIB). Makenga alikimbilia Uganda na kuwekwa chini ya uangalizi.
Hata hivyo, jina lake limeendelea kutajwa katika mijadala ya usalama mashariki mwa DRC, hasa kufuatia kufufuka tena kwa harakati za M23 kuanzia mwaka 2022.
Tangu 2022, Makenga ametajwa kuwa miongoni mwa watu wanaotafutwa zaidi na mamlaka ya Kinshasa. Taarifa zinaeleza kuwa kumekuwa na operesheni kadhaa za kumkamata bila mafanikio.
Katika tukio la hivi karibuni lililoripotiwa Jumanne, mapigano makali yalidaiwa kuhusisha wanajeshi wa AFC/M23, ambapo Luteni Kanali Willy Ngoma alifariki dunia. Hata hivyo, Makenga anaripotiwa kutokuwepo eneo la tukio, na alibaki mahali pasipojulikana.
Drone zimeshafika Congo haijajulikana Mfadhili gani ameipatia Jeshi la Serikali ya Congo Drone hizo, wengi wanasema.huu ndio mwisho wa M23.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG