BANDA MEDIA BLOG

WASTARA ATANGAZA NDOA NA DUDUBAYA


 Penzi la Wastara(43) na Dudubaya(51) limeanza kuchukua sura mpya baada ya Wastara kutoa kauli inayodokeza tayari amepanga kufunga ndoa na Dudubaya ambaye ni mwanamuziki mkongwe wa kizazi kipya(Bongofleva). Wastara ndie alianza kuweka wazi penzi lao kisha Dudubaya kuthibitisha baadaye

Wastara ambaye baba yake alikuwa muarabu, hata hivyo haijajulikana bado ndoa ya safari hii wamepanga iwe ya dini gani kwani yeye Wastara ni muislamu wakati Dudubaya ambaye jina lake halisi ni Godfrey Tumaini, ni mkiristo

ITAKUWA NDOA YA NNE

Wastara ambaye alizaliwa mwaka 1983, alipokuwa shule ya secondary kidato cha pili aliacha shule huko Morogoro, akiwa na miaka 16 aliolewa na mwanaume kutoka Zanzibar ambaye alimzidi sana umri ingawa ndoa haikudumu ilivunjika ndani ya muda mfupi

Baada ya kufanya kazi pamoja katika filamu kadhaa, 2008/2009 Wastara alifunga ndoa ya pili na Sajuki aliyekuwa mwigizaji wa filamu, hadi Sajuki alipoaga dunia 2013, walijaaliwa mtoto mmoja

January Mwaka 2016, Wastara aliolewa na Sadifa Juma aliyekuwa mbunge wa jimbo la Donge, Zanzibar hata hivyo ndoa yao haikudumu waliachana, hawakupata mtoto pamoja

Wastara ana watoto wengine akiwemo mmoja aliyezaa na Solo Thang mwanamuziki mkongwe wa hip-hop Tanzania ambaye kwasasa anaishi Ulaya kwa miaka takribani ishirini. Penzi lao lilikuwa mwanzoni mwaka miaka ya 2000s kabla hajaanza na Sajuki

Mbali na hayo, Wastara aliwahi pia kuwa katika mahusiano na Bond Suleiman mtangazaji na mwigizaji wa Kibongo kabla hajaolewa ghafla ndoa ya tatu hali ikiyosababisha Bond kukiri kutaka kujiu@ baada ya mrembo huyo kwenda kuolewa na mwanaume mwingine 

Kwa upande wa Dudubaya alishawahi kuwa na mke kabla, pia ana watoto kutoka mahusiano yake ya awali

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG