BANDA MEDIA BLOG

CCM SASA YAWAITA WENYE MIGOGORO YA NDOA

 



KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi, amesema CCM ipo tayari kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, ikiwemo migogoro ya ndoa.

Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha amani na maelewano katika familia, kwa kuwa kazi ya chama tawali ni kuhakikisha umoja na amani vinakuwepo. 

Kauli hiyo ameitoa leo, baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa maduka 60 na vizimba 69 vya biashara katika soko la Bukokwa, uliogharimu zaidi ya Sh.million 577, uliopo Halimashauri ya Buchosa, wilayani Sengerema. 

Amesema mbali na kusikiliza na kutatua  changamoto za wananchi, yupo tayari pia kupokea na kusaidia kutatua migogoro ya kifamilia inayoweza kuvuruga ustawi wa jamii.

"Kama kuna ndoa imetetereka njooni niambie, tuiweke sawa tunataka kila mtu aishi kwa amani na furaha, hata kama mke wako anakupiga njooni tuzungumze kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Nyehunge” alisema.

 

Aliongeza kuwa jamii yenye amani na maelewano ndani ya familia huchangia ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa na eneo husika.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG