BANDA MEDIA BLOG

DKT. MWINYI, DKT NCHIMBI NA DKT MPANGO KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 5 YA KIFO CHA HAYATI MAGUFULI

 


GEITA; MAKAMU wa Rais wa Tanzania Dk Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka mitano ya kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli. 

-Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela alitoa taarifa hiyo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari na kueleza maadhimisho hayo yatafanyika Machi 17, 2026, wilayani Chato. 

-Shigela alisema Dk NchimbI anatarajiwa kuwasili mkoani Geita leo mchana kupitia uwanja wa ndege wa Chato. 

-Alisema misa na maadhimisho hayo yatahudhuriwa pia na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ambaye atawasili mkoani Geita kesho. 

-Alitaja viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria shughuli ya maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mstaafu, Dk Philip Mpango na Waziri Mkuu mstaafu, Kassim Majaliwa. 

-Alisema tukio hilo limeratibiwa na familia ya Dk Magufuli kwa kushirikiana na serikali, ambapo litatanguliwa na misa takatifu. 

-Alisema misa hiyo ya kumuombea na kumuenzi itafanyika nyumbani kwake Chato na kuongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi.

- Alisema maadhimisho yataanza rasmi leo kwa matukio mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na mbio zitakazoanza asubuhi kuelekea Hospitali ya Wilaya ya Chato.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG