Kisarawe.
Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe Dkt Selemani Said Jafo Leo 14/03/2026 amefunga Rasmi Mashindano ya kuhifadhi na Kusoma Quran tukufu Juzuu 1-15 kwa Mwaka 2026 yalioandaliwa na jumuia ya waislamu Kisarawe JUWAKI,
Akizungumza leo katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Minaki amesisitiza kulinda amani na utulivu wa nchi ya Tanzania pamoja na kuendelea kumuombea Mhe Rais Dkt Samia katika majukumu yake ya Kila siku ya ujenzi wa Taifa,
*"Ndugu zangu waTanzania tuwe na Imani na utu na utulivu maana Dunia imeharibika Sana Sisi tunapokua na Imani na kumjua mwenyezi mungu tunakua Salama hivyo basi tuwe na utamaduni wa kuwaombea Dua wazazi na Viongozi wetu katika jamii wasipatwe na kiburi"* alisisitiza MHE DKT JAFO
Nae Mkurugenzi wa jumuia ya waislamu Kisarawe JUWAKI sheikh Waziri Pazi Amesisitiza waislamu Kisarawe kuwaunga mkono wanafunzi wa madrasa na walimu mbalimbali pindi wanapopatwa na matatizo ikiwemo miundombinu khafifu ya madrasa,
*"Unakuta madrasa ni mbovu na hafifu sehemu ambayo anatajwa mwenyezi mungu haifai nawaomba wazazi na walezi wajitolee katika kusimamia maboresho ya miundombinu mbalimbali ya madrasa zetu Kisarawe,*" alisisitiza sheikh Pazi
Kadhalika Sheikh wa Wilaya Kisarawe Bakwata Sheikh Ramadhani Kumbangulu akimuakilisha Sheikh wa mkoa wa Pwani katika mashindano hayo amesisitiza amani na utulivu katika jamii kuelekea siku ya Eid-Ftri.
Jumla ya madrasa 30 katika kata 7 na wanafunzi walishiki 345 mashindano ya Mwaka huu 2026 kwa Juzuu 1-15.

