BANDA MEDIA BLOG

DR Congo: Raia waandamana Goma kulalamikia ukosefu wa usalama

DR Congo: Raia waandamana Goma kulalamikia ukosefu wa usalama

Jijini Goma,mashariki mwa DRC, kumefanyika maandamano baada ya shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani siku ya Jumatano na kusababisha vifo vya watu watatu, akiwemo raia wa Ufaransa  mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNICEF, linaloshughulikia masuala ya watoto.


 Na:


Wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali kuomba amani,maelfu ya raia hao, walikusanyika katikati mwa mji wa Goma kabla yakuelekea kwenye ofisi ya tume ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini kongo,Monusco .

Kwa mujibu wa waandamanaji hao, hatua hiyo imechochewa na wito kutoka kwa baadhi ya makundi ya kiraia, wakisema kuwa ni wakati  wakukomesha  mashambulizi ya droni kwenye  miji na vijiji nchini Kongo.

 “Tunaandamana kutokana na mashambulizi ya droni katika mikoa ya kivu kaskazini na kusini. Serikali ya kinshasa imetuzarau saana kwakutuwa. Tunacho kitaka ni amani tu.” Walisema baadhi ya waandamanaji.

Maandamano ya kulalamikia kuongezeka kwa utovu wa usalama Goma.
Maandamano ya kulalamikia kuongezeka kwa utovu wa usalama Goma. REUTERS - Stringer

Wakati wengi wao wakitembea kwa miguu wengine waliamua kuandamana kwa utumia usafiri wa  pikipiki japokuwa baadhi walieleza kutojua sababu yao kuandamana. Kwa saa kdhaaa, shughuli zilisimama huku biashara zikisitishwa kwa kipindi hicho.

Maandamano haya yanakuja siku moja tu baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani, ambalo lilitokea katikati ya jiji la Goma na kusababisha maisha ya  watu watatu, akiwemo mfanyakazi wa shirika la UNICEF na raia wa Ufaransa .

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG