BANDA MEDIA BLOG

PONGEZI KWA UONGOZI WA KLABU YA YANGA SC CHINI YA RAIS ENG. HERSI SAID

 


NA DENIS MLOWE, IRINGA 

MCHEZAJI wa zamani wa Klabu ya Young Africans Sports Club, Ally Msigwa, ametuma pongezi kwa viongozi wa klabu hiyo akiwapongeza kwa mafanikio makubwa ambayo wameyafanikisha chini ya uongozi wa Rais wa klabu hiyo, Eng. Hersi Said.

Akizungumza na Full Shangwe Media, Mkoani Iringa , Bw. Ally Msigwa Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa sasa, klabu imepiga hatua kubwa ndani na nje ya uwanja na kuendelea kuonesha ubora ambao umeifanya kuwa miongoni mwa timu bora zaidi barani Afrika. 

Amesema kuwa Chini ya uongozi huo, Yanga imefanikiwa kutwaa mataji ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), na pia kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa kwa kufika hatua za juu katika Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msigwa ameongeza kuwa maboresho ya kiutawala, nidhamu ya kifedha na usajili uliolenga kuongeza ushindani uwanjani yamechangia kuipa Yanga nguvu mpya na kuonyesha kuwa uongozi huo una dira ya kuipeleka klabu mbali zaidi. 

Pia ametaja heshima ambayo klabu imepata kimataifa kupitia nafasi mbalimbali alizochaguliwa kuongoza Eng. Hersi Said, ikiwemo ile ya Mwenyekiti wa Chama cha Vilabu Afrika (ACA) na ujumbe katika Kamati ya Mashindano ya Soka la Wanaume Duniani ya FIFA.

Katika kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi wa klabu, Msigwa ametoa rai kwa wanachama kutambua mchango wa uongozi uliopo na kuwawekea mazingira ya kuendelea na kazi, akisema kuwa uthabiti na mafanikio yaliyopo ni matokeo ya uongozi makini unaostahili kuendelezwa. 

mebainisha kuwa Yanga inaendelea na mipango mikubwa ya maendeleo, ikiwemo hatua za awali za ujenzi wa uwanja wa kisasa katika eneo la Jangwani.

Aidha, ametoa pongezi kwa wadhamini wakuu ambao wamekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya klabu, akiwataja GSM na SportPesa kwa mchango wao katika kuimarisha uwezo wa kifedha wa timu hiyo.

Msigwa pia ameishukuru Kamati ya Wadhamini, matawi ya klabu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, pamoja na mashabiki na wanachama wa Yanga SC kwa kuendelea kuiunga mkono timu kwa njia mbalimbali, ikiwemo kuhudhuria mechi, kununua bidhaa rasmi na kulipia ada za uanachama.

Amesema kuwa mafanikio ya klabu yanatokana na umoja wa wadau wote na kuwataka kuendelea kushikamana ili Yanga iendelee kuwa juu na kufikia mafanikio makubwa zaidi katika siku zijazo.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG