BANDA MEDIA BLOG

IRAN YAIVURUMUSHIA MAKOMBORA ISRAEL MUDA MFUPI BAADA YA KUTANGAZWA KIINGOZI MKUU MPYA WA DALA YA KIISLAMU

Iran imefanya shambulio lake la kwanza la makombora dhidi ya Israel leo Jumatatu, muda mfupi baada ya kumtangaza Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei kuwa Kiongozi Mkuu mpya wa Jamhuri ya Kiislamu.
Shambulio hilo limeandamana na kauli mbiu ya kishia “Kwa Amri Yako, Sayyid Mojtaba,” sambamba na picha za makombora zikionyesha uungaji mkono wa kijeshi na wa kiimani chini ya uongozi mpya.
Wakati mvutano ukiongezeka, Qatar imetoa wito mkali wa kupunguza vita na kuweka silaha chini, kabla haijawa nje ya udhibiti katika eneo zima la Mashariki ya Kati.

HII HAPA HISTORIA FUPI YA KIONGOZI HUYU

Ayatollah Mojtaba Khamenei Ndiye anakuwa kiongozi mkuu wa Iran 'Rahbar Imam' wa Tatu, ambaye Alizaliwa katika mji wa Mashhad katika familia ya Khamenei, baba yake Ali Hussein Javad Khamenei ndie alikuwa kiongozi Mkuu wa Pili wa Iran toka Mwaka 1989.
Mojtaba Khemenei ni kutoka kabila la Azeri kwa baba na Kiajemi kwa Mama, haya makabila ni muhimu sana kwenye Siasa na ushawishi wa kisiasa nchini Iran.
Alipata elimu ya awali huko Sardasht na Mahabad, na akahitimu sekondari jijini Tehran, kisha akajiunga na elimu ya dini chini ya mwanzuoni mkubwa wa kishia aliyeitwa Mahmoud Hashemi Shahroudi.
Mwaka 1987 alijiunga na jeshi la ualinzi la Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na mwaka huo huo akaenda kushiriki vita ya Iran na Iraq mwaka 1987, Mwaka 1999 aliamua kuendelea na masomo ya dini na kuamua kujiunga na chuo cha Qom seminar, hiki chuo ndio kisima cha maarifa yote ya Kishia duniani na ni eneo linaloheshimika kwenye taaluma na kutoa wanazuoni mashuhuri ulimwenguni kwenye elimu ya dini ya Kiislamu.
Mwaka 2009 Mojtaba Khemenei alichaguliwa kuwa kiongozi wa Kikosi maalum cha "Basij" kikosi cha kijasusi kilicho chini ya kikosi cha IRGC, lakini toka 1999 alikuwa ni naibu mnadhimu wa kamati ya ulinzi na siasa, kamati hiyo inafanya kazi chini ya kiongozi mkuu wa Iran.
Mojtaba Khemenei ni mwanazuoni wa dini aliyebobea kwenye falsafa ya "Usuli" yani misingi ya dini inayo pendelea matumizi ya "ijtihad" (hoja) katika uundaji wa sheria mpya za kidini katika kutathmini hadithi ili kuondoa mila wanazoamini wengi kuwa haziaminiki.
Mojtaba Khemenei ni mtu mwenye misimamo mikali sana, ni miongoni mwa "Iranian Principlists" katika siasa za Iran, ni moja ya waliokuwa wakiunga mkono Iran itengeneze nuklia katika mjadala ulioibuka mwaka 2007 na kuzimwa na Fatwah ya baba yake Ayatollah Ali Khamenei aliyepiga marufuku Iran kutengeneza silaha za nyuklia.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG