Mchezaji wa kimataifa wa Iran na mshambuliaji wa klabu ya Ugiriki Olympiacos F.C. na ambaye hapo awali aliwahi kuichezea FC Porto pamoja na Inter Milan, Mehd Taremi, amewajulisha viongozi wa klabu yake ya sasa kuhusu nia yake ya kurejea nchini kwao ili kusimama bega kwa bega na uongozi wa jeshi na makamanda wa kijeshi, kwa lengo la kushika silaha na kuitetea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Maafisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Iran wanajaribu kumshawishi mchezaji huyo abaki nchini Ugiriki, lakini mshambuliaji huyo wa Iran amejibu kuwa huu ndio wakati ambao nchi yake inamhitaji zaidi.
Tags
VITA