.......................................
Mratibu wa Utume na Uinjilisti Kanda ya
ziwa wa Kanisa la Angilikana Tanzania Rev Happyness Ndunguru Chanai amewapongeza
wanawake zaidi elfu 25 waliokutanika kwenye kongamano la Maombi Duniani
lililofanyika Mkoani Kagera.
Amesema Kongamano hilo limezaa matunda ya
Wokovu kwa wanawake 700 huku wengine wakipokea miujiza ya uponyaji na baraka za
Mungu, huku akiwataka wanawake hao kutunza wokovu pamoja na miujiza waliipokea
kwa kuendelea kumtafuta Mungu kwa njia ya maombi na kujifunza zaidi neno la
Mungu..
Mratibu wa Utume na Uinjilisti Kanda ya ziwa wa Kanisa la Angilikana Tanzania Rev Happyness Ndunguru Chanai
“kupata wokovu, miujiza ni jambo moja ili
kuvitunza lazima udumu katika maombi na kujifunza neno la Mungu kwa bidi ili
uendelee kukua kiroho”, amesema
Kongamano hilo ambalo hufanyika kila
mwaka ki Dunia mwezi kama huu, limewakutanisha wanawake wa kanisa hilo kanda ya ziwa katika
Dayosisi ya Kagera chini ya Askofu
Darlington Bandankeha huku likiongozwa na neno kutoka kitabu cha Mathayo 11:28
Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha.
“hakika Mungu ametupumzisha, amefanya
mambo makubwa kwa wanawake wa kanda ya ziwa, jina la Bwana libarikiwa"



