Rais wa Shirikisho la Soka la Kongo (FECOFOOT), Jean Guy Blaise Lionel Mayolas, amehukumiwa kifungo cha maisha siku ya Jumatatu, Machi 9, na Mahakama ya Jinai ya Brazzaville. Mahakama ya Kongo inamhusisa, pamoja na wanachama kadhaa wa shirikisho, kughushi na kutumia hati bandia, kuchukua riba kinyume cha sheria, na kushiriki katika ushiriki wa uhalifu huo.
Alipopatikana na hatia, Jean Guy Blaise Lionel Mayolas alihukumiwa kifungo cha maisha, kama mmoja wa wanawe. Hukumu hiyo pia inajumuisha faini ya faranga milioni 100 za CFA, au takriban euro 152,000.
Uchunguzi ulibaini kuwa Mayolas alitumia karibu dola milioni 1.3 za fedha za FIFA kwa manufaa yake binafsi, na kutumia mtandao wa miamala ya kifedha ya bandia na rekodi za uwongo kuficha ukweli huo.
Sambamba na hilo Mke na mtoto wa Mayolas wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na makosa hayo huku Katibu Mkuu wa FECOFOOT, Badji Mombo Wantete, na Mhasibu, Raoul Kanda, wakihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja.
Hukumu iliyotolewa bila mtuhumiwa kuwepo
Hukumu hiyo ilitolewa bila mhutuhumiwa kuwepo, kwani rais wa FECOFOOT hakuonekana kwenye kikao cha kesi, inaripoti redio ya umma ya Kongo. Hati ya kukamatwa imetolewa dhidi yake, na kwa sasa anatafutwa.
Mashtaka ya ubadhirifu na utakatishaji fedha yanaanzia janga la Covid-19. Kulingana na uchunguzi, zaidi ya dola milioni moja katika fedha zilizotengwa na FIFA zilidaiwa kuibwaa na maafisa wakuu wa shirikisho.
Katibu mkuu wa FECOFOOT, Bandji Mombo Wantété, na mhasibu, Raoul Kanda, kila mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na kutozwa faini ya faranga za CFA milioni moja. Wote wawili walikuwepo kwenye kikao hicho.
Hakuna tangazo lililotolewa kuhusu uwezekano wa uongozi wa muda wa shirikisho.