BANDA MEDIA BLOG

WATU WAMEZOOM SMS ZA CHIEF NA PIPI


 Pipi joji ni msanii ambaye  Watu wengi walimjua kwa uzuri wake, kipaji chake cha kuimba na sauti yake ya kipekee iliyowavutia mashabiki wengi.

Katika safari yake ya muziki, kulikuwa na mtu mmoja aliyejitolea sana kumsaidia na kumsimamia. Mtu huyo aliitwa Chief Godlove. Chief Godlove aliamini sana kipaji cha Pipi Joji, hivyo akachukua jukumu la kuwa meneja wake.

Alipigania kila kitu ili kuhakikisha msanii huyo anafanikiwa. Alimtafutia nafasi, alimsaidia kurekodi nyimbo na hata kumtangaza kila mahali. Kwa pamoja walifanya kazi kwa bidii sana mpaka wakatoa nyimbo kadhaa zilizopendwa na watu wengi, ikiwemo wimbo maarufu wa Chakacha ambao uliwafanya watu wengi kuanza kumtambua zaidi.

Lakini kadri siku zilivyokuwa zinaenda, mambo yakaanza kubadilika. Kulianza kuibuka maneno mengi na tetesi mbalimbali kuhusu uhusiano wao wa kazi.

Ghafla siku moja, Chief Godlove alitangaza rasmi kuwa kuanzia siku hiyo ameachana na Pipi Joji na hatakuwa tena meneja wake. Tangazo hilo lilishtua mashabiki wengi na watu wa media.

Vyombo vingi vya habari vilianza kumtafuta Pipi Joji ili waelewe kilichotokea hasa, lakini msanii huyo hakuzungumza chochote kuhusu sababu ya kuondoka kwake. 

Siku moja, wakati Pipi Joji akiwa anatoka zake nje, mtu mmoja alimchukua picha kwa mbali. Picha hiyo iliposambaa mtandaoni, watu walianza kuizoom sana ili kuona vizuri kile kilichokuwa kwenye simu yake.

Walipoizoom zaidi, ndipo wakaona ujumbe uliokuwa umeandikwa kwenye simu yake.

Baada ya watu kuuona ule ujumbe, wengi walishika vichwa vyao kwa mshangao na kutikisa vichwa, wakijiuliza maswali mengi zaidi kuhusu kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia.

Kupitia huo ujumbe unahisi nini kimefanya watu washangae?

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG