Na:
Ofisi ya kiongozi huyo wa mashtaka imesema, inachunguza tukio hilo, ili kubaini waliohusika katika shambulio hilo ambalo limeelezwa ni uhalifi wa kivita.
Uchunguzi huo umeanza dhidi ya watu hao wasiofahamika waliohusika katika tukio hilo ambalo limezua wasiwasi wa kiusalama miongoni mwa wakaazi wa mjio huo wa Goma, unaodhibitiwa na waasi wa M23/AFC tangu Januari mwaka uliopita.
Kwa kawaida, raia wa Ufaransa anapouawa nje ya nchi, mamlaka katika nchi yake huchunguza, mazingira yaliyosababisha kuuawa kwake, na kuona uwezekano wa kuchukua hatua na kuomba ushirikiano kwa nchi husika.
Katika hali hii, viongozi wa mashtaka watawasikiliza mashahiri, na kuomba pia ushirikiano wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO ili kubaini ukweli wa kilichotokea na kusababisha kifo cha Karine Buisset.