BANDA MEDIA BLOG

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA SOKO LA KISASA LA MAZAO KANONDO-RUKWA

 

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, Machi 8, 2026 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kisasa la Mazao Kanondo lililopo Sumbawanga mkoani Rukwa.

‎Ujenzi wa soko hilo unatekelezwa kupitia Mradi wa TACTIC kwa gharama ya shilingi bilioni 7.3, na hadi sasa umefikia asilimia 82 ya utekelezaji.

‎Soko hilo linatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mazao, likiwaunganisha wakulima, wanunuzi wakubwa, wasafirishaji na wawekezaji, hatua itakayopanua mtandao wa biashara na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wa Rukwa na maeneo jirani.   

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG