BANDA MEDIA BLOG

KUNA UTOFAUTI GANI KATI YA DHAMBI NA MAKOSA?- MWINJILISTI SEMBUCHE


Kuna tofauti gani kati ya Dhambi na Makosa?  ni swali hili linaloulizwa kwako na Mwinjilisti wa Kanisa Anglikana Tanzania Magreth Sembuche, ambaye amesema tatizo la watu wengi ni kutokujua kutofautisha, ndiyo sababu ya wengi kujikuta wakitumbukia katika dimbwi hilo...

Bi. Magreth anesema vitendo vinavyotokea kwa udhaifu wa kibinadamu, kujua au kutojua na hata kutokuwa Makini, ni sababu zinapelekea jamii zetu kuingia matatizoni kila uchwao.

Akitoa Mfano,  Martha kwenye kitabu cha Luka  10: mst 40,43 inayosema kuwa,

"Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie,

41 Bwana akajibu akamwambia, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;

42 lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa. 

    Alikuwa na shughuli nyingi na akasahau kilicho muhimu kusikiliza,hii haikuwa dhambi ya moja kwa moja, bali ni kosa",

Bi Magreth anasema Dhambi ni kukosa kwa makusudi huku ukijua sio sahihi, 

Akaongeza mfao wa dhambi waliotenda Adam na Eva Bustanini Eden ambao walijua kula tunda ni dhambi, pia Mfalme Daudi kulala na     Bathsheba huku akipanga mbinu za kumuua mume wake hizi ni dhambi za makusudi 

"Mfano Adamu na Eva walikula tunda la mti wa katikati huku wakijua walishaonywa hivyo walifanya kusudi, ukiacha hao hata mfalme Daudi kulala na mke wa Askari wake, huku akipanga kumuua Mumewe si kuwa hakujua kuwa ni kosa bali ilikuwa ni makusudi yaliyosumwa na tamaa ya mwili", amesema

Aidha amesema wengi wetu tumekuwa tunafanya makosa pamoja na kutenda dhambi si kwamba hatujui ila tunasukumwa na hisia za tamaa za kimwili, huku tukisongizia ubinadamu

Magreth akaomgeza  kuwa katika yote Mungu ametupa neema kama inavyosomeka kwenye 1 Yohana 1:9  kwamba Tukiziungama dhambi zetu, Mungu ni mwaminifu na wa haki hata  kutusamehe.

Swali lipo pale pale, je Kuna tofauti Gani kwako kati ya Dhambi na makosa, je unakisea au kutenda dhambi bila kujua,  tumbie hapa!!! 

Magreth Sembeche ni FOUNDER WA HUDUMA YA REHEMA NA NEEMA

magrethchilingosembuche@gmail.com

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG