Akiwa na umri wa miaka 11, Osman Ali DavutoÄŸlu tayari ameanza kuonesha dalili nzuri katika mchezo wa kale nchini Uturuki.
Amezaliwa nchini Tanzania, Osman alifiliwa na wazazi wake wawili na kuasiliwa na aliyekuwa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoğlu pamoja na mke wake, Yeşim Meço Davutoğlu.
Mwaka 2020 walirudi nchini Uturuki. Ilikuwa ni msimu wa kiangazi Balıkesir ambapo kwa mara ya kwanza alijaribu mchezo wa mieleka ya kupakwa mafuta.

Akwa na familia yake, alifanya mazoezi, na ghafla uwezo wake kuonekana. Hivi sasa, Osman anajinasibisha na ‘Arab Mustafa’ Yıldız, bingwa wa mieleka mwenye asili ya Kiafrika na Uturuki kutoka Manisa.
Ndoto yake: kushinda shindano la mieleka ya mafuta la Kırkpınar na kujishindia jina la mwana mieleka bora.
Anasema yeye amehamasishwa na mwanzilishi wa Jamhuri ya Uturuki, Mustafa Kemal Atatürk, Mustafa Yıldız, na bingwa wa mieleka Mustafa Taş na kwamba anaona "fahari kubwa" kushirikia katika mashindano ya Kırkpınar.

