BANDA MEDIA BLOG

Ripoti ya UN yalaumu mitandao ya kigeni kwa kuchochea vita vya Sudan

 

Umoja wa Mataifa unasema kwenye ripoti yake siku ya Alhamisi kuwa mitandao ya kigeni yanachochea katika vita nchini Sudan ambavyo vimeendelea kati ya jeshi na wapiganaji wa kundi la RSF tangu 2023, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 59,000, na kuwaondoa kama milioni 13 katika makazi yao.

Inasema mtandao wa mashirika yaliyoko nje ya nchi umechangia wapiganaji wa kijeshi, silaha na mafunzo kwa RSF.

“Uchunguzi huo umebaini sababu za kuamini kuwa mtandao uliwapa RSF silaha, mafunzo na wapiganaji wa kigeni, ikiwemo wale wanaohusika na silaha za kisasa na mifumo ya droni,” kulingana na muhtasari wa uchunguzi wa Volker Türk, Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu.

Ilibaini kuwa watu fulani walioko nje ya nchi "wanahusika na mitandao ya kusajili watu, kufadhili, kusafirisha na kuwafikisha wapiganaji wa kigeni pamoja na kutoa usaidizi wa kijeshi unaowafaidi RSF.”

Wachunguzi wametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza muda wa marufuku ya silaha kwa Sudan.

“Silaha, ufadhili, wanajeshi na teknolojia ambazo zinasaidia katika vita lazima zizuiwe,” inasema.

Pia walihusisha wapiganaji wa kigeni waliopewa mafunzo nje ya nchi na mauaji ya kikatili ya 2025 katika kambi za Zamzam na El Fasher.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG