LESONI LEO, SEPT 13-VITA VYA KIROHO
Paulo anakutana na dharau na upinzani katika kanisa la Korintho tena. Na dharau hizo/upinzani huo unaibuka baada ya watu (walimu wa uongo) na baadhi ya watu katika namna fulani inavyoonekana, kusema/kuibua mjadala kwamba 👉 barua alizokuwa akiandika akiwa mbali zilikuwa barua nzito, za ujasiri na za maonyo makuu. Lakini alipokuwa akikutana na Wakorinto uso kwa uso, Paulo hakuonekana kama ambavyo Wakorinto walikuwa wamempiga picha kupitia barua zake. Na hivyo, kanisa, kutokana na hoja hizo 👉 likachukulia upole wa Paulo kama udhaifu na kuanza kusema maneno kama vile, Paulo hakuwa na nguvu ya kweli, wala hakuwa akijiamini kama ilivyokuwa katika barua zake. Upinzani ukaibuka tena hata baada ya wao kutubu kutokana na waraka mzito wa Paulo tuliokwishakuuona katika masomo yaliyotangulia!!
Lakini je, ni kweli Paulo alikuwa dhaifu?! Huu upole wake ulimaanisha nini?! 👇👇👇
- Paulo hakuwa dhaifu. Angeweza kushughulika na Wakorinto katika namna hiyo wanayotaka (ya kwenye barua) hata uso kwa uso. Tunajua angeweza, maana hapo nyuma kabla hajaja kwa YESU alishughulika na watu katika namna hiyo. Unakumbuka jinsi Paulo alivyowatesa watu wa MUNGU, akiwafunga na kuwapeleka gerezani, akidhani kwamba alikuwa anafanya jambo sahihi? Hivyo aliweza. Na hata sasa anasema hivi katika barua yake kwa Wakorinto (rejea 2 Wakorinto 10) kwamba anaweza kuwa hivyo hivyo pia uso kwa uso kama itamlazimu kuwa hivyo kwa ajili ya wokovu wao.
Isipokuwa Paulo hakufanya hivyo wakati alipokuwa nao uso kwa uso hapo awali. Kwa nini?! Kwa sababu alitambua kuwa kanisa linapitia vita ya kiroho. Na huu mchezo wa vita ya kiroho 👉 hahuitaji hasira. Kuna wakati ukitumia hasira, ukali, vitisho 👉 unaweza kukuta unawaangamiza wengi kuliko unavyodhani. Haimaanishi kwamba wakati wote tuwe wapole, la hasha! Kuna wakati wa kusimama kwa ujasiri bila woga, lakini kuna wakati ili uweze kuokoa, inatakiwa kushuka, naam kushuka na kunyenyekea kabisa. Hivyo alijua ni vita ya kiroho na ndiyo maana alishuka. Wewe fikiria tu katika hili analoshughulikia sasa. Ni ndiyo kwanza tu ametoka kutuma waraka mzito na watu wakatubu kutokana na waraka huo mzito (tuliona). Halafu sasa, watu wametubu mara akiwa bado yuko huko huko mbali zinaibuka hoja nyingine tena. Hoja za kwamba, "anaweza tu kwa barua. Lakini uwepo wake kimwili ni dhaifu na usemi wake si kitu". Kama si vita hii ni nini?! 😊. Hakika ilikuwa ni vita kubwa ya kiroho ya kuwarudisha nyuma kanisa la Korintho.
Ukitaka kujua ninachomaanisha, mkumbuke YESU msalabani, ili kutuokoa, ilimpasa kunyenyekea na kuwa mpole mpaka mauti. Shetani alimchochea YESU atumie nguvu zake kwa mateso mengi, alimlazimisha YESU apandwe na hasira kwa dharau nyingi na kejeli nyingi-Lakini YESU alichagua kutokufanya hivyo. Je, inamaanisha kwamba hakuwa na uwezo huo?! La hasha. Alikuwa nao. Lakini hakufanya hivyo. Kwa sababu kutumia nguvu zake, kungezuia mpango wa wokovu kwa mwanadamu. Kwa ajili ya kutuokoa, naam akavumilia mateso, akawa mpole na mnyenyekevu mpaka mauti.
Na kama tujuavyo, hapo awali aliikemea dhambi kwa ujasiri na kwa ukali. Kumbuka tukio la hekaluni, jinsi YESU alivyowakabili kwa ujasiri wale waliokuwa wakifanya biashara hekaluni na kuzipindua meza zao (Mathayo 21:12–13). Kumbuka jinsi alivyowakabili kwa ujasiri viongozi wa kidini (Mafarisayo) akiwaita wanafiki na “makaburi yaliyopakwa chokaa,” kwa sababu walionekana wazuri kwa nje lakini ndani walikuwa wamejaa uchafu. Lakini anapofika msalabani, pamoja na kejeli zote, pamoja na matusi yote, pamoja na dharau zote, pamoja na maumivu yote, pamoja na mashinikizo yote ya adui shetani 👉 YESU anakuwa mnyenyekevu, naam, mnyenyekevu mpaka mauti kwa ajili yetu.
Hicho ndicho Paulo anachojaribu kutufundisha katika somo la leo na ndicho anachojaribu kuwaambia Wakorinto. Kwamba yeye siyo mdhaifu isipokuwa vita vya kiroho havipiganwi kwa mapanga, bunduki na hasira 👉 badala yake vinapiganwa kwa silaha za kiroho (upole, maombi, Neno la MUNGU, utii, upendo, utu wema n.k). Siyo kwamba ni mdhaifu isipokuwa vita vya kiroho wakati wote havitumii silaha moja tu. Kuna wakati itahitaji kuwa hodari, jasiri, kuitaja dhambi kwa jina lake bila kuogopa na kusimama upande wa kweli bila kuyumba (hali ambayo wakati fulani inaweza kufanya wakuchukulie mkali na unayetisha sometimes 😊 kutokana na tafasiri ya shetani vichwani kwa watu 😊).
Lakini kuna wakati itakuhitaji kunyenyekea kama siyo wewe, kuna wakati itakuhitaji kuonekana mjinga, zuzu. Kuna wakati itakuhitaji kuonekana kama aliyechanganyikiwa. Kuna wakati itakuhitaji kuonekana mshamba na wa zamani 😊, kuna wakati itakuhitaji kuonekana namna gani vipi 😊. Kuna wakati itakuhitaji kusimama upande wa kweli hata kama watu watakuona kama adui yao 😊.
Hivyo Paulo hakuwa na udhaifu kama wapinzani wake walivyokuwa wakinena. Bali alikuwa akionesha kuwa anaweza kuwa jasiri (bold) na mpole vile vile!!! Bali alikuwa akiwataka Wakorinto watambue kuwa kuna wakati wa kusimama kwa ujasiri na kuna wakati wa kushuka-Na alipokuwa mpole, ilikuwa ni wakati wa kuwa hivyo. Na alipokuwa bold ilikuwa ni wakati wa kuwa hivyo. Bali alikuwa akiwataka Wakorinto wasichukulie upole wake anapokuwa nao kama udhaifu. Ni kama vile Paulo alikuwa akiwaambia Wakorinto hivi, "Upole si udhaifu, na ujasiri si ukali. Katika vita vya kiroho, tunahitaji hekima ya kujua wakati wa kusimama kwa ujasiri na wakati wa kunyenyekea kwa upole".
Nikuache na swali hili?! Unafikiri ni katika wakati gani tunapaswa kuwa majasiri, wasioyumba na watu wasioogopa kuitaja dhambi kwa jina lake?! Unafikiri ni wakati gani ambao tunapaswa kuruhusu watu wafikirie kama wanavyofikiria wenyewe 👉 kwamba sisi ni kama adui zao, tuko kinyume chao na wakati fulani wakali kama ambavyo wanadhani wao?! Na kwa upande mwingine wa shilingi unafikiri ni wakati gani tunapaswa kuwa wapole?! Watiifu? Naam wanyenyekevu mno 👉andika jibu lako kwenye Comment hapo chini tujifunze pamoja.
