Alichosema Fabregas Kuhusu Kuongoza Mgomo Dhidi Ya Mourinho
byJohn Banda-
0
Baada ya kuzuka kwa tuhuma kwamba yeye ni mmoja wa wachezaji wanaoongoza
mgomo wa wachezaji wa Chelsea dhidi ya kocha wap Jose Mourinho – kiungo
Cesc Fabregas ameamua kutoa yake ya moyoni juu ya shutuma hizo.
Cesc Fabregas kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter mchana huu
amekanusha taarifa zilizotolewa wikiendi iliyopita kwamba yeye ndio
mchezaji aliye mbele kupinga mbinu za ufundishaji za Jose Mourinho
Kiujgo huyo umri wa miaka 28 amekanusha na mgomo baridi unaoripotiwa
kuwepo Stamford Bridge na kuongeza kwamba ana mahusiano mazuri sana na
mwalimu wake na amesema kuna watu wa nje ya klabu wanajaribu kutengeneza
mazingira ya ugomvi ndani ya klabu.
Hatua ya kiungo huyo kuongea hadharani itatuliza hali ya sintofahamu baina ya mashabiki na wachezaji.Hata hivyo kujitetea kwa Fabregas kutapelekea mchezaji mwingine
kupewa zigo la lawama ya kuongoza mgomo ambao unatajwa sana kuwepo ndani
ya timu.