Frank Mvungi, MAELEZO
Rais mteule wa Jamhuri Ya
Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa
kushinda kiti cha Rais katika uchaguzi mkuu ulifanyika oktoba 25, 2015
ikiwa ni kielelezo cha utendaji bora alionyesha katika kuwatumikia
watanzania kupitia nyadhifa alizotumikia kabla ya kuchaguliwa katika
nafasi hiyo.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu Chama cha Mapinduzi
(CCM) Bi Zainab Abdallah wakati wa mkutano na waandishi wa Habari
uliolenga kumpongeza Rais mteule kwa tiketi ya chama hicho.
“Akifafanua Bi Zainab amesema
kuwa Rais Mteule Dkt. John Pombe Magufuli ameshinda kiti cha Urais kwa
kuwa ndiye mtu pekee ambaye watanzania walikuwa wanamuhitaji ili aweze
kuwaletea maendeleo kwa kuwa ni mchapa kazi na ameonyesha kwa vitendo
dhamira hiyo katika utumishi wake kwa miaka yote iliyopita “alisisitiza
Zainab
Bi. Zainab amesema kuwa Rais
mteule Dkt. Magufuli anayo dhamira ya dhati yakuwaletea maendeleo
watanzania ndiyo sababu hata kauli mbiu yake ililisisitiza kuwa “hapa
kazi tu” hivyo ni wajibu wetu kama watanzania kusisitiza umoja na
mshikamano na kuondoa tofauti zetu ili tufanye kazi kwa bidii ili
kujenga uchumi wa taifa.
Akizungumzia wasifu wa Rais
Mteule Dkt. Magufuli; Bi Zainab amesema kuwa ni mtu mwenye
uzalendo,mwadilifu,mchapa kazi, na ambaye watanzania wote wanamkubali
kuwa anao uwezo wa kuliongoza Taifa katika kipindi hiki.
Kwa upande wa Uchaguzi mkuu
Zainab amesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki hali iliyowapa
nafasi watanzania kuchagua viongozi wanaowataka na kupelekea chama cha
mapinduzi kuongoza katika uchaguzi huo kutokana na utendaji madhubuti
wa viongozi wa Chama na Serikali.
Pia Bi Zainab alitoa wito kwa
watanzania kudumisha amani na umoja wa Kitaifa ulioasisiwa na Viongozi
wa kwanza wa Taifa hili ili kufikia maendeleo ya Kweli.
Shirikisho la wanafunzi wa vyuo
vikuu Chama cha Mapinduzi (CCM) limekuwa likihamasisha vijana kufanya
kazi kwa bidii ili kujenga Taifa.
Tags
SIASA

