Waendesha mashtaka wanaouchunguza
matukio ya mashambulio ya kigaidi mjini Paris Ufaransa wamemtaja mmoja
wa washambuliaji 7 wa kujitoa mhanga.
Omar Ismail Mostefai mwenye umri wa miaka 29 anasemekana kuwa
ni raia wa ufaransa aliyekuwa anachunguzwa na polisi wa kupamabana na
ugadi kabla hajatoweka.
Mtu huyo tayari alikuwa na rekodi ya uhalifu.
Omar ametambuliwa kutokana na kidole kilichopatikana katika eneo la tukio.
 |
Kiongozi wa mashtaka wa Ufaransa Francois Molins
Uchunguzi pia utalenga kubaini iwapo aliwahi kusafiri kwenda Syria au la .
Wachunguzi
hao wanasema washambuliaji hao walijipanga katika vikundi vitatu kabla
ya kutekeleza mashambulizi hayo kwa mabomu na ufyatuaji wa risasi.
Mbali
na bunduki washabuliaji hao pia walikuwa na mikanda ya mabomu
waliotumia kujilipua katika msururu huo wa mashambulio yaliyosababisha
vifo vya watu 129.
Wengi wa waliolengwa walikuwa mashabiki wa tamasha la muziki, wateja katika migahawa ,baa na hata mashabiki wa soka.
Kundi la wanamgambo wa I S wamedai kuhusika na tukio hilo |
 |
Rais wa Ufaransa ametangaza hali ya hatari na kufunga kabisa mipaka ya taifa hilo.
Washambuliaji 7 walijilipua huku mmoja wao akipigwa
risasi wakati wa operesheni ya kuokoa maisha ya watu waliokuwa ndani ya
ukumbi huo wa maonyesho.
Wachunguzi wanasema kuwa wanahofu kuwa washambulizi zaidi waliotoroka na sasa msako unaendelea.
Rais wa Ufaransa ametangaza hali ya hatari na kufunga kabisa mipaka ya taifa hilo. |