BANDA MEDIA BLOG

REAL MADRID YATOTA DHIDI YA SEVILLA WAKATI NEYMAR AKIING'ARISHA BARCELONA

Klabu ya Soka ya Real Madrid ya nchini Hispania imekutana na kipigo cha kwanza katika ligi ya La Liga msimu huu cha mabao 3-2 kutoka kwa Sevilla katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania uliopigwa jana usiku.

Wakiwa ugenini Madrid walianza kupata bao lililofungwa na Sergio Ramos lakini Sevilla wakafunga mabao matatu kupitia Cillo Immobile, Ever Banega na Fernando Lloriente huku bao la pili kwa Real Madrid likifungwa na James Rodrigues.

Kipigo hicho kwa Madrid kinaiacha Barcelona kutamba kileleni kwa pointi 27, pointi tatu mbele ya Real Madrid baada ya jana vijana wa Jose Henrique kuibuka na ushindi wa nabao 3-0 jana usiku dhidi ya Villarreal.
Sergio Ramos akisikilizia maumivu ya bega baada ya kufunga bao kwa mtindo Bicycle Kick.

  Neymar akifurahia bao alilofunga

Luis Suarez akifurahia bao la penati alilofunga



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG