Vikosi vya ulinzi shirikishi vikipokea maelekezo ya namna ya kukabiliana na uhalifu katika kipindi hiki cha sikuku za mwisho wa mwaka.
Kila mmoja ni vizuri akatambua kuwa usalama unaanza na yeye mwenyewe na maana
halisi ya sikukuu hizi ni kumtukuza Mungu na kudumisha amani na pale
watakapotilia shaka jambo lolote watoe taarifa Polisi ili kupatiwa msaada wa
haraka. Ninawatakia sikukuu njema zenye amani na utulivu.
![]() |
| Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime akitoa maelekezo namna ya kukabiliana na uhalifu kipindi cha sikuku za Chrismas na Mwaka mpya nje ya jengo la polisi mkoa |
![]() |
| Magari ya polisi yatakayotumika katika ulinzi |
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma tumejipanga kikamilifu katika
kuhakikisha Maadhimisho ya sikukuu katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka 2015
na mwanzo wa mwaka 2016. Siku kuu zinazotarajiwa kusherehekewa ni MAULID
itakayofanyika katika Misikiti mbalimbali tarehe 24/12/2015 itakayofuatiwa na
Mkesha wa X- Mass katika Makanisa mbalimbali hadi siku yenyewe ya X- Mass
tarehe 25/12/2015 na hatimaye tarehe 01/01/2016 Sikukuu ya mwaka mpya.
Tutaimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya biashara na
mikusanyiko ya watu. Tutafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya
dola ili kuhakikisha yeyote mwenye nia ovu ya kufanya uhalifu wa aina yeyote
anadhibitiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada na makampuni
ya ulinzi binafsi nao washiriki kikamilifu ili kuhakikisha ulinzi unaimarika na
ibada zinafanyika bila bughudha ya aina yeyote.
Wanacnhi wote wakazi wa Dodoma na wageni
watakao kuwa hapa Dodoma katika kipindi hiki cha siku kuu za mwisho na mwanzo
wa mwaka kuchukua tahadhari za kiusalama, washerehekee kwa amani na utulivu na shamra shamra zao zisivunje sheria.
Wazazi
wahahikikishe watoto wao hawaendi katika kumbi za starehe na bar bali
wanasherehekea
katika mazingira salama wakiwa chini ya uangalizi makini, ulinzi
majumbani
uimarishwe wasiache nyumba peke yake. Wamiliki wa kumbi za starehe
wahakikishe hawajazi watu kupita kiasi, wahakikishe usalama ni wa
kutosha katika kumbi zao.
Aidha watumiaji wote wa barabara wazingatie sheria za usalama
barabarani na hasa waendesha vyombo vya moto wazingatie udereva wa kujihami na
kuhakikisha kwenye makazi ya watu hawaendeshi vyombo vya moto zaidi ya spidi
50kph kama sheria za usalama barabarani kifungu cha 51 kinavyoelekeza. Kuepukana
na ulevi kupita kiasi na kutoendesha magari wakiwa wamelewa ili kuepusha ajali
zisizozalazima.
Tags
HABARI KITAIFA





