BANDA MEDIA BLOG

WANAWAKE WA LANGO WATAKIWA KUACHA TABIA YA KUWAPIGA WANAUME ZAO

Kiongozi wa jamii ya Lango nchini Uganda Dk. Michael Odongo Okune amewaonya wanawake wa kabila la Langi kuhusiana na tabia ya kuwapiga wanaume wao kutokana na vitendo hivyo kuongezeka mno.

Akiongea na waombolezaji kwenye maziko ya Rose Omona Odyebo wilyani Oyam, Dk. Odongo amesema viongozi wa kimila wa Lango hawatovumilia ukatili na vipigo katika ngazi ya familia vinavyofanywa na wanawake ama wanaume.

Dk. Michael Odongo Okune ambaye pia ni Waziri wa Kimila wa Lango ameonyesha kukerwa na vitendo vya wanawake wa kabila la Langi kuwadunda wanaume zao, hali inayochochea vurugu kwenye familia.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG