Jana habari kubwa kwa wapenda soka wote ilikua ni kuhusu
mtanzania Mbwana Samatta kujiunga na club ya KRC Genk akitokea TP
Mazembe. Mbwana amekua mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kujiunga na
club hii ambayo inashiriki ligi kuu ya Ubeligiji.
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na
michezo Nape Nnauye alikua bega kwa bega na Mbwana Samatta kabla na
baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Africa kwenye CAF Glo Awards.
Baada ya jana habari za Samatta kusajiliwa na Genk kumfikia,Nape Nnauye ametumia page yake ya twitter kuandika “Serikali tulipoamua kumsaidia, tulisemwa tumeanza udalali, leo matunda ya “udalali” haya hapa! ”.
Serikali imempa support Mbwana Samatta hata kabla hajawa
mchezaji bora wa Africa tangu alivyokua Congo ambapo Rais Jakaya Kikwete
alienda kumtembelea alivyokua ziarani na kuongea nae maneno ambayo
Samatta anasema yaliwatia moyo yeye na mwenzake Ulimwengu.
Tags
MICHEZO KITAIFA