BANDA MEDIA BLOG

MWANAMKE AMUUA MPENZI WAKE KUTOKANA NA UGOMVI WA RIMOTI

Polisi Kenya inamshikilia mwanamke anayedaiwa kumuua mwanaume wake kwa kumchoma kisu, kufuatia ugomvi uliosababishwa na mvutano wa kuangalia programu za televisheni.

Kamishna wa Polisi wa Nairobi Kaunti Japhet Koome, amesema mwanamke huyo wa miaka 27 aitwae Caroline alimchoma mpenzi wake mwenye umri wa miaka 25 siku ya jumanne usiku.

Bw. Koome amesema wapenzi hao wawili walikuwa wanagombea remoti kila mtu akitaka kuangali programu tofauti na ndipo mwanamke alipochukua kisu jikoni na kumchoma nacho mwanaume tumboni na kwenye paja.

Ugomvi huo ulitokea saa nne usiku wakati chaneli moja televisheni ilipokuwa ikionyesha tamthilia na nyingine ikionyesha mechi ya mpira miguu.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG