Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu barani Asia (AFC) na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin
Ebrahim Al Khalifa amewasili nchini leo mchana na kupokelewa na Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Sheikh Salman amekuja nchini kwa matembezi ya siku ya mbili na atakua na mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Kesho Jumanne, Sheikh Salman Bin
Ebrahim Ali Khalifa atamtembelea ofisini Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel.
Tags
MICHEZO KITAIFA