Kiungo wa Chelsea Ramires amekamisha usajili
wake wa kujiunga na klabu ya China Jiangsu Suning kwa ada ya uhamisho
inayoaminika kufikia £25m.
Mbrazil huyo mwenye miaka 28 amekubali mkataba mpya wa miaka minne
lakini alipata nafasi ya kuanza kwenye mechi saba pekee za Premier
League msimu huu.Jiangsu iliyomaliza ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimu wa mwaka 2015 inanolewa na beki wa zamani wa The Blues Dan Petrescu.
Ramires aliisaidia Chelsea kushinda mataji ya Premier League, FA Cup, League Cup, Champions League pamoja na Europa League.
Akiwa Chelsea Ramires alicheza mechi 251 akafanikiwa kufunga mabao 34 tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Benfica kwa kitita cha pauni milioni 17 hiyo ilikuwa ni mwaka 2010
Tags
MICHEZO KIMATAIFA