Kikao maalum cha menejimenti ya
Tume wakijadili vipaumbele muhimu kwaaajili ya utekelezaji wa majukumu
yake ya kila siku baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015
Baadhi ya watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika kikao hicho.
Na Mwandishi-NEC
Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza kupitia vipaumbele kwa ajili ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017.
Katika kikao chake cha
Menejimenti kilichofanyika leo Januari 11, 2016, baadhi ya vipaumbele
vinavyoendelea kujadiliwa ni uhuishaji wa Sheria mbalimbali
zinazosimamia masuala ya uchaguzi, Elimu ya Mpiga Kura, na ujenzi wa
ofisi ya Tume.
Vipaumbele vingine
vinavyojadiliwa ni pamoja na miongozo na mifumo ya ufuatiliaji na
tathmini, mifumo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na
mifumo ya uendeshaji wa Uchaguzi.
Tume imeanza mandalizi haya ili
kujipanga vema ili mwongozo wa Bajeti utakapotoka, Menejimenti ya NEC
iwe imekamilisha hatua zote za awali na kusubiri kuwasilisha katika
ngazi husika.
Huu ni utaratibu mpya
ulioanzishwa na Tume ya Uchaguzi ili kuhakikisha masuala yote muhimu
yanakuwepo katika uandaaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Vikao hivi vya Menejimenti ya
Tume ni vikao vya kawaida vinavyofanyika kila Jumatatu kwa ajili ya
kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa kila Idara na kujipanga
kwa utekelezaji wa wiki inayoanza.
Tags
SIASA