John Obi Mikel alifunga goli muhimu wakati wa mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya Chelsea ikiwa ugenini dhidi ya PSG kwenye uwanja wa Parc des Princes, Ufaransa.
Bao hilo lilikuwa ni la pili kwenye michuano ya Ulaya kwa kiungo huyo wa Nigeria ambaye jana usiku akiwa kwenye eneo sahihi kwa wakati sahihi aliifungia Chelsea bao la kusawazisha dakika ya 45 baada ya PSG kupata bao lao la kwanza kupitia kwa Zlatan Ibrahimovic.
Mikel alifunga goli lake la sita katika kipindi chote ambacho amekuwa mchezaji wa Chelsea takribani miaka 10 sasa
January 6, 2007 v Macclesfield
Goli la kwanza la Mikel akiwa mchezaji wa The Blues lilikuwa kwenye mchezo wa FA Cup mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Macclesfield kwenye uwanja wa Stamford Bridge. Mchezo huo ulimalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa bao 6-1 huku goli la Mikel likiwa ni la 5 kwenye mchezo huo.
January 28, 2007 v Nottingham Forest
Mabeki wa Forest walishindwa kuudhibiti mpira wa kona uliopigwa na Frank Lampard ambao ulitua kwenye miguu ya Mikel ambaye alikukwamisha moja kwa moja kambani na kuiandikia Chelsea bao la tatu kabla ya half-time kwenye mchezo uliomalizika kwa Chelsea kushinda magoli 3-0.
September 21, 2013 v Fulham
Baada ya zaidi ya miaka 6 bila goli, Mikel alitupia bao lake la kwanza kwenye Premier League akiunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na John Terry kutokana na krosi ya Lampard. Goli hilo lilikuwa ni la pili kwenye ushindi wa magoli 2-0.
January 5, 2014 v Derby
Mikel alifunga kwa kichwa goli lake la nne akiwa Chelsea kwenye mechi yake ya 300 wakati Chelsea inapata ushindi wa bao 2-0.
December 10, 2014 v Sporting Lisbon
Mikel alifunga bao lake la kwanza mwenye michuano ya Ulaya wakati Chelsea ikipata ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Sporting Lisbon.
Video ya goli la John Obi Mikel kwenye mchezo wa UEFA Champions League PSG vs Chelsea February 16, 2016