BANDA MEDIA BLOG

KUELEKEA YANGA SC V SIMBA SC, ‘TAMBWE+NGOMA=24’ VS ‘KIZZA +AJIB=24’ KAZI KWA MABEKI


Hassan Isihaka wa Simba akijaribu kuzuia mpira usitoke nje ya uwanja mbele ya Donald Ngoma wa Yanga wakati wa mchezo wa watani wa jadi Septemba 26, 2015
Hassan Isihaka wa Simba akijaribu kuzuia mpira usitoke nje ya uwanja mbele ya Donald Ngoma wa Yanga wakati wa mchezo wa watani wa jadi Septemba 26, 2015
Na Baraka Mbolembole
Donald Ngoma na Amis Tambwe kwa pamoja wamekwishafunga jumla ya magoli 24 msimu huu wakiwa na timu yao ya Yanga SC. Upande mwingine, Hamis Kizza na Ibrahim Ajib pia wamekwishatupia kambani jumla ya magoli 24 katika VPL hadi sasa, kwa maana hiyo tunaweza kusema ‘washambuliaji hao wanne wanalingana katika magoli.’
Kuelekea mechi ya mahasimu hao wa soka nchini (Yanga v Simba) siku ya Jumamosi hii ni wazi kuwa kila upande una washambuliaji wa kutosha kuwa ushindi. Itakuwa ni kazi ya mabeki sasa kuweza kumaliza mechi.
Safu ya ulinzi itakayocheza vizuri na kwa nidhamu itakuwa na mchango mkubwa katika timu husika kuhakikisha ushindi unapatikana.

Yanga walijilinda vizuri na kushambulia vizuri katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba. Na licha ya kujaribu kucheza vizuri, Simba ilifungwa kutokana na udhaifu wa safu yao ya ulinzi ambayo ilikuwa chini ya Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Juuko Murishid na Mohamed Hussein ‘Tshabala.’
Yanga itamkosa mlinzi wake wa kati Kelvin Yondan anayetumikia adhabu, pia huenda nahodha, Nadir Haroub asitumike katika mchezo huo kutokana na kwamba hakuwa fiti kwa muda mrefu kutokana na majeraha ya mguu.
Mlinzi wa kushoto Mwinyi Hajji hajaonekana katika michezo minne iliyopita ya ligi kuu kutokana na majeraha aliyokuwa nayo na hivyo alitoa nafasi kwa Oscar Joshua kucheza katika beki ya upande wa kushoto.
Karibu safu yote ya ulinzi iliyocheza katika mchezo wa mzunguko wa kwanza waliposhinda 2-0 inaonekana kuyumbishwa na sababu mbalimbali, na wakati huu Kizza na Ajib wakionekana kutengeneza ushirikiano mzuri.
Yanga watasumbuliwa katika beki kama tu machaguo ya Hans van der Pluijm hayatakuwa sahihi. Hans si kocha muoga, anaweza kumuweka benchi Nadir na kuwapa nafasi ya kucheza pamoja Mtogo, Vicent Bossou na Mnyarwanda, Mbuyu Twite kusimama katika beki ya kati. Oscar na Juma Abul katika fullbacks.
Lakini watafaa kwa safu hii ya sasa ya mashambulizi ya ‘Kizza+Ajib=24’? (usikose uchambuzi wangu wa gemu hii) ‘Tambwe+Ngoma=24’ inaongezewa makali na Saimon Msuva ambambaye amekwishafunga magoli sita msimu huu.
Hajji Ugando upande wa Simba anaweza kuwa mchezaji wa tatu mkali na wa kuchungwa na walinzi wa Yanga na Msuva atakuwa msumbufu wa tatu wa Yanga kwa safu ya ulinzi ya Simba.
Hii ni mechi inayowakutanisha washambuliaji wenyewe viwango vya juu kiufungaji, ni kuwatazama tu mabeki jinsi watakavyokuwa wakihaha kuzibeba timu zao.
Yanga SC v Simba SC, ‘Tambwe+Ngoma=24’ vs ‘Kizza +Ajib=24’ kazi kwa mabeki.

CHANZO NI SHAFFIHDAUDA.COM

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG