Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel ameitumia
salamu za Rambirambi familia ya Mzee Dellan Tarmo kufuatia kifo cha
kijana wao mpendwa Jovitha Dellan kilichotokea kwa ajali ya gari mkoani
Arusha juzi tarehe 31.1.2016.
“Pokea rambirambi zangu za dhati, sote kwa pamoja tumepoteza kijana mchapakazi, hodari na aliyepen
da kushirikiana na wenzake katika kazi zake, hakika tutamkumbuka siku zote” Katibu Mkuu amesema.
da kushirikiana na wenzake katika kazi zake, hakika tutamkumbuka siku zote” Katibu Mkuu amesema.
Katibu Mkuu, Pia amemtumia salamu
za pole kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu(KBF) na Wafanyakazi wote
wa Bodi ya Filamu Tanzania.
“Nimepokea taarifa za kifo
cha Jovitha Dellan kwa huzuni kubwa, najua machungu na maumivu mliyonayo
kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika utendaji wenu, poleni sana,
niko nanyi katika msiba huu mzito kwenu”, amesema Katibu Mkuu huyo.
Katibu Mkuu amesema pamoja na
kwamba kifo hakiepukiki, bado ni kitu ambacho kinashtua, kuhuzunisha na
kuleta unyonge mkubwa kwa wafiwa katika jamii.
“Naungana nanyi katika
kipindi hiki kigumu kumuombea kijana wetu Jovitha Dellan ili mwenyezi
Mungu ampe mapumziko mema ya Milele” Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape uvumilivu na subira katika kipindi hiki”.
“Niko nanyi katika kipindi hiki kigumu kwa hali na mali, nawaomba msijisikie wapweke” Katibu Mkuu amesema na kuwatakia utulivu na amani katika kipindi hiki cha msiba mkubwa kwa familia.
Marehemu Jovitha Dellan
amefariki juzi tarehe 31 Januari, 2016 mkoani Arusha ambapo alikuwa
njiani kurejea kazini jijini Dar es salaam.
Marehemu Jovitha Dellan anatarajiwa kuzikwa wiki hii mkoani Manyara .
Jovitha Dellan alikuwa ni Afisa Utamaduni aliyekuwa akifanya kazi
katika Bodi ya Filamu Tanzania iliyopo chini ya Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Jovitha Dellan mahali Pema Peponi, Amina.
Tags
HABARI KITAIFA