Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa
Habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kikao na uongozi wa TBC
leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC Clement
Mshana.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikpokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. Clement Mshana aliupowasili
katika ofisi za TBC Mikocheni leo jijini Dar es Salaam..
………………………………………………………………………………
Na: Frank Shija, WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili
wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC kutokana na utendaji usioridhisha.
Akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape
amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya
Habari na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi Bibi. Edna
Rajab ambao wote kwa pamoja wasimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa
kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi.
“ Tunachukua uamuzi
wakuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu
katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla” Alisema Nape
Aidha Waziri huyo amemuagiza
Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine walio chini
ya Idara hiyo kwakuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho wa
hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonyesha utendaji mbovu.
Alisema kuwa Serikali imefikia
uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu juu ya
utendaji mbovu na wakutoridhisha viongzi na baadhi ya watumishi wa Idara
hiyo hiyvo hatua hizo zimechukuliwa ikiwa ni kujenga upya na kuboresha
Idara hiyo muhimu katika uendeshaji wa Shirika lolote lile la Habari na
kuongeza ufanisi.
Idara ya Habari na Matukio ya TBC
inaundwa na Mkurugenzi wa Idara, Meneja wa Vipindi Wahariri na
Waandishi wa Habari ambapo tayari Mkurugenzi na Meneja wa Vipindi
wamesimamishwa kazi leo tarehe 15 Februari 2016 na watumishi wengine
watachukuliwa hatua kufuatia agizo la Mhe. Waziri wa Habari kwa
Mkurugenzi Mkuu wa TBC alilolitoa leo wakati akitangaza kuwasimamisha
kazi viongozi hao.
Tags
HABARI KITAIFA