Wanachama
wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Manispaa ya Ilemela Mkoani
Mwanza, leo wamefunga Ofisi ya Taasisi ya Mikopo ya WADOKI (Wadoki
Saccos) pamoja na Hotel ya KIRUMBA RESORT kutokana na watajwa kushindwa
kulipia kodi ya pango.
Mwenyekiti
wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid (anaeongea pichani) amesema kuwa
wanachama hao wamefikia maamuzi hayo kutokana na kutumia majengo ya CCM
katika kata hiyo huku wakiwa hawalipii kodi.
Wanachama
wa CCM katika Kata hiyo ya Kirumba wamesema kuwa, maamuzi yao yatatoa
fundisho kwa wawekezaji wengine wanaotumia vitega uchumi vya Chama hicho
katika maendeo mbalimbali nchini huku wakiwa hawalipii kodi ambapo
wametahadharisha kwamba wale wote wenye hulka hiyo wajiandae kutumbuliwa
(kuondolewa katika majengo hayo).
Katibu
Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Juma Wesa pamoja na Katibu wa Chama
hicho Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi, wamesema kuwa maamuzi
yaliyochukuliwa na wanachama hayo ni sahihi kwa kuwa malalamiko ya
wawekezaji hao yaliishajadiliwa hadi ngazi za juu na kuonekana kwamba
wawekezaji hao hawatii makubaliano yao ikiwemo kulipa kodi ya pango kwa
wakati.
Meneja
wa Kirumba Resort hakutaka kuzungumzia malalamiko hayo kwa madai kwamba
mzungumzaji ni Mkurugenzi ambae alidai amesafiri huku Uongozi wa Wadoki
Saccos ukishindwa kupatikana.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Acheni Maulid akitoa kwa wanaccm baada ya wanachama hao kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Katibu
wa CCM Wilaya ya Ilemela, Acheni Maulidi akizungumza baada ya wanaccm
kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii
leo
Katibu
Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Wesa Juma, akizungumza baada ya wanaccm
kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii
leo
Jane
Masso ambae ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Kirumba (kulia)
amesema wanachama watahakikisha vitega uchumi vya chama vinatumika vyema
kwa ajili ya maendeleo yao.
Mmoja wa wanaccm akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Mmoja wa wanaccm akizungumza baada ya wanaccm kufunga Ofisi ya Wadoki Kirumba pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, hii leo
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya Hotel ya Kirumba Resort, hii leo baada ya kuifunga kutoa huduma
Ofisi ya Wadoki Saccos Kirumba baada ya kuwekewa kama ishara ya kufungwa
Ulinzi
wa Askari wa Kutuliza ghasia ulikuwepo ili kuhakikisha hakuna uhalibifu
wowote ambao ungeweza kufanyika ambapo suala hilo limefikishwa Kituo
cha Polisi Kirumba na kila upande unawasilisha vielelezo vyake ili
kutambua wanaokiuka makubaliano ya mkataba wa upangaji.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group
Tags
BIASHARA