Papa Francis amewaambia wafungwa
katika gereza la wafungwa hatari nchini Mexico wawe manabii na
kutumia uzoefu wao wa kukaa katika hali ngumu gerezani kubadili hulka
ya ghasi nchini humo.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki
Duniani ametoa ombi hilo kwa wafungwa wa Ciudad Juarez, mji ambao
uliowahi kujulikana kama mji wa mauaji, ikiwa ni siku chache tu
kupita tangu ghasi za gereani kusababisha vifo vya wafungwa 49 nchini
Mexican.
Papa Francis akipokea msalaba uliochongwa na mmoja wa wafungwa nchini Mexico
Tags
KIMATAIFA

