Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitoa ufafanuzi juu ya Wizara yake kuhakikisha itapeleka Madaktari bingwa katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo hospitali hiyo ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema Februari 13.2016.
Kauli
hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii
Jinsia na Watoto mjini Songea, Dkt. Hamisi Kigwangalla baada ya kufanya
ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kituo
cha afya cha Mjimwema kilichopo mjini Songea huku akiitaka mikoa ya
pembezoni ukiwemo mkoa huo wa Ruvuma kuweka mazingira ya kuwavutia
madaktari bingwa kufanya kazi katika mikoa yao.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu amesema kuwa mkoa
huo umeridhishwa na staili ya ziara ya kushtukiza na kwamba
wanajitahidi kuboresha vituo vya afya vya Mjimwema Songea, Madaba na cha
wilaya ya Namtumbo ili vipandishwe hadhi kuwa hospitali za wilaya.
Pia
Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kutembelea maeneo mbalimbali ya
Hospitali hiyo na kujionea utendaji wa kazi huku akitoa wito katika
suala la maboresho zaidi.
Imeandaliwa na Andrew Chale wa Modewjiblog, Ruvuma.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (katikati) akijiandaa kuingia kukagua utendaji wa kazi na vifaa ndani ya chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake hiyo Februari 13.2016.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akijiandaa kuingia kwenye chumba cha upasuaji wakati wa ziara yake hiyo, aliyoifanya mapema Februari 13.2016.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vitanda vinavyotumika katika upasuaji hospitalini hapo ambapo hata hivyo aliambiwa changamoto kuwa baadhi ya taa za vitanda hivyo kuwa na hitilafu wakati ziara hiyo mapema Februari 13.2016. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Songea, Ruvuma)
Tags
AFYA