BANDA MEDIA BLOG

ZAIDI YA WAKULIMA 60 WAKIJIJI CHA MAPINDUZI 'A' KATA YA NGHONG'ONHA, MANISPAA YA DODOMA WANAHOFU YA KUPOTEZA MASHAMBA YAO YENYE UKUBWA WA HEKARI 237, NA MWANAKIJI MWENZAO MWENYE FEDHA




Moja ya Kaburi lililopo katika Mashamba hayo yenye Mgogoro katika ya wakazi wa Mapinduzi na Mwenzao kijini hapo, Kaburi hilo lilizikwa mwak 1958

Baadhi ya wakulima wa Kijiji cha Mapinduzi wakiwa wamekusanyika katika Eneo la Mgogoro ambalo walikuwa wakilitumia kwa kilimo.



Joyce Fundi miaka 982) mwenye Jembe akieleza jambo kuhusu Makaburi hayo na Jinsi shamba lake pamoja na ya wakulima wengine yalihatalini kutaifishwa. IMETENGENEZWA NA BANDA BLOG
  Na Lydia Kishia, Dodoma
ZAIDI ya Wakulima 60 wa Kijiji cha Mapinduzi ‘A’ kata ya Nghong’onha  manispaa ya Dodoma wanawasiwasi wa kunyang’anywa mashamba yao yenye ukubwa wa Hekari 237 kutokana na mkazi mwenzao aliye na nia ya kuwadhulumu kwa vitisho vya kutumia polisi ikiwemo kuburuzwa mahakamani huku wakikosa msaada wowote toka kwa viongozi wa ngazi za juu.
Wakulima hao wakiwa mashambani
Wakizungumza na waandishi wa habari Kijijini hapo wakulima hao walisema wamekuwa wakipata wakati mgumu tangu mwaka 2012 ambapo Bwana Mchiwa Chedego alipowaomba wamuuzie mashamba ili ayatumie kwa kilimo cha zabibu wakamkatalia na ndipo akaanza visa vya kuwakamata na kuwapeleka kwenye mabaraza ya ardhi ngazi za kijiji na kata ambako walishinda na baadae akawahamishia Wilayani.

Walimesema kuwa mkazi huyo anayejulikana kwa jina la Mchiwa Chedego ambaye anataka kuwadhulumu eneo lao amekuwa akiwaleta wawekezaji na kuwaonyesha eneo hilo bila hata ya kuujulisha uongozi wa kijiji hicho

Pia wamewaomba viongozi wanaohusika na masuala ya Ardhi kufika katika kijiji hicho na kuchunguza eneo hilo kwani haiwezekani eneo lote la kijiji hicho likawa la mtu mmoja na wakati hata wazazi wake walikuwa hawana eneo kubwa kama hilo
 
Wananchi hao wamesema kuwa Chedego amekuwa akifungua kesi mara kwa mara mahakamani kwa lengo la kutaka kuchukua eneo hilo kwa nguvu kutokana na yeye kuwapa fedha polisi  na huku wao kushindwa kesi kwa kuwa ni maskini na hawana fedha za kuwapa polisi hao

Kwa upande wake mwenyekiti wa  kijiji hicho Willy Joseph amemuomba mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya  kuingilia kati mgogoro huo na kuweza kuutatua kwani ndilo eneo ambalo wakulima hao wanajipatia kipato cha kukidhi mahitaji yao muhimu

Nae Diwani wa Kata ya Nghon’oha Philip Namga alisema kuwa Mgogoro huo ameukuta ni wa Muda mrefu sasa lakini hawezi kuuzungumzia kwa kuwa shauri hilo lipo mahakama ya Wilaya lakini kwa sasa anamsubiri Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthon Mavunde ambaye kwa sasa Yupo jijini Dar es Laam kwa shuhuli za kiserikali ili afikishie Taarifa hiyo ili ajue jinsi ya kuwasaidia wapiga kura wake.

Bado juhudi za kumapata Chedego ili aweze kutoa ufafanuazi wa Tuhuma dhidi yake zinaendelea kutokana na kutokuwepo kijijini hapo wakati waandishi walipofanya ziara kijijini hapo.
 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG