Pluijm amezungumza mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na imani yake ya kufuzu kwenda hatua inayofuata ya michuano ya klabu bingwa Afrika, kukosekana kwa Juma Abdul na hali za wagonjwa Said Makapu pamoja na Matheo Anthony.
Juma Abdul ataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya APR kutokana na kuoneshwa kadi mbili za njano kwenye michezo miwili mfululizo, lakini kama mchezaji mmoja au wawili wanakosekana unawaleta wachezaji wengine kuziba nafasi. Unawapa hali ya kujiamini na kitu kizuri ni kwamba tumeanza mazoezi mapema Jumanne tangu tuliporejea.
Said Makapu na Matheo Anthony wao wanasumbuliwa na Malaria lakini hadi kufikia Jumamosi tunaamini watakuwa wamepona.
Tutacheza kwa kushambulia pale itakapobidi na tutajilinda tutakapotakiwa kufanya hivyo kwenye mchezo wetu wa Jumamosi. Kwenye michuano hii hasa hatua za kutafuta kufuzu kwenda hatua zinazofuata unatakiwa kushambulia sana.
Kama tutacheza kwa kujituma na kujiamini ninauhakika tutapata matokeo mazuri kwasababu tayari tumeshaonesha kwenye mchezo wa ugenini, vilevile siyo lazima kushinda mchezo wa nyumbani lakini tumejiandaa kisaikolojia na ninaamini tutafanikiwa siku ya Jumamosi na kusonga mbele.
Tags
MICHEZO KITAIFA