Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu,Sera na Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua akizungumza na wajumbe wa
kamati ya maafa ya taifa(TANDTRADE)( Hawapo pichani) wakati wa kikao cha
kamati hiyo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Katiba na Sheria Amon Mpanju akifatilia kikao cha Kamati ya Maafa ya
Taifa kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni katibu wake.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya
Maafa ya taifa kutoka katika Wizara,Taasisi na Idara za Serikali
wakifatilia kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa kilichofanyika leo Jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya
Maafa ya taifa kutoka katika Wizara,Taasisi na Idara za Serikali
wakifatilia kikao cha Kamati ya Maafa ya Taifa kilichofanyika leo Jijini
Dar es Salaam.
Picha zote na Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
…………………………………………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Serikali imekusudia kuanzisha
Wakala wa Usimamizi wa Maafa Tanzania chini ya Sheria ya mwaka 2004
ambao utakuwa na jukumu la kupambana na maafa yatakayojitokeza kwa
kuratibu na kuwezesha waathirika wa maafa kupata misaada ya mahitaji
muhimu kwa haraka.
Akizungumza na wajumbe wa Kamati
ya Maafa ya Taifa(TANDTRADE) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na
Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua amesema Serikali imedhamiria kuanzisha
Wakala wa Usimamizi wa Maafa ili kuweka utaratibu mzuri ambao utasaidia
kushughulikia kwa umakini maafa yatakayokuwa yakijitokeza katika sehemu
mbalimbali nchini.
“ Ipo Sheria ya Wakala wa
Usimamizi wa Maafa basi ni jambo jema kuwepo kwa Wakala ili kuweza
kuratibu vizuru shughuli za kupambana na maafa yanayotukumba”
“Tumekutana leo hapa katika kikao
cha kawaida cha kupata taarifa juu ya maafa yanayotokea nchini na
tutajadili na kutoa madhimio ambayo yatatoa majibu ya nini kifanyike
katika kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa kupambana na maafa”
Alisema Dkt Mwinyimvua.
Kamati ya Maafa ya Taifa iko
chini ya mwenyekiti ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na
Uratibu ikiwa na wajumbe kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa, Wizara ya
Afya,Ustawi wa Jamii,Watoto na Wazee, Jeshi la Zima Moto,Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Taasisi na
Idara za Serikali zinazohusika na maafa.
Tags
HABARI KITAIFA