Mhe. William Lukuvi akipokea
msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa kutoka kwa Bibi Sawidath
Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA)
tawi la Dar es salaam akiwa na Bibi Rose Majuva Kamishna wa Makao
Makuu ya Taasisi hiyo (wa pili kulia) na Grace Shaba Naibu Katibu Mkuu
TGGA.
Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti
wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es
salaam akimkabidhi Mhe. William Lukuvi msaada wa Wahanga wa mafuriko
Isimani Iringa.
Baadhi ya vitu alivyopokea Mhe.
Lukuvi kwa ajili ya wahanga hao vikiwa katika gari ambavyo ni Chakula,
Nguo , viatu na Madaftari.
Mhe. William Lukuvi akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ofisini kwake.
………………………………………………………………………………………………………
Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi apokea Msaada kwa Wahanga
wa mafuriko Iringa. Msaada huo ni kutoka Taasisi ya Tanzania Girl
Guides Association (TGGA) ambayo imemkabidhi Mhe. Lukuvi Unga kilo 155,
Nguo na viatu balo 2, Sukari kilo 25 na Madftari Boksi 2 kwa ajili ya
wahanga wa mafuriko jimboni kwake Isimaani.
Taasisi ya TGGA ni shirika lisilo la Kiserikali na ni chama cha kujitolea kinachojishughulisha na kuwaendeleza Wanawake pamoja na Watoto wa kike katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo
Taasisi ya TGGA ni shirika lisilo la Kiserikali na ni chama cha kujitolea kinachojishughulisha na kuwaendeleza Wanawake pamoja na Watoto wa kike katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo
Tags
HABARI KITAIFA