Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi
wengine na wananchi wakibeba jeneza la Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi
wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya
kuswaliwa leo wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika Kijijini kwao Donge
wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Wananchi waliohudhuria katika mazishi ya Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM wakilibeba jeneza wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitia udongo
katika kaburi la Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM baada ya kufariki jana katika
hospitali ya Mnazi Mmoja na kuzikwa leo Kijijini kwao Donge wilaya ya
Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na wananchi
na Viongozi wakiwa katika maziko ya Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi
wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM aliyezikwa leo
Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakiitikia dua
iliyoombwa baada ya kuzikwaMarehemu
Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee
wa CCM leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja,[Picha na
Ikulu.]
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed akisoma risala na wasifu wa Marehemu
Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee
wa CCM baada ya kuzikwa leo Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini
B.Unguja,[Picha na Ikulu.]
…………………………………………………………………………………………..
Maelfu ya wananchi wakiongozwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein leo wameshiriki mazishi ya mmoja ya waasisi wa Mapinduzi ya
Zanzibar Mzee Hamid Ameir.
Mzee Hamid Ameir ambaye alifariki
jana katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar ambako alilazwa
kwa matibabu amezikwa kijiji kwao Donge wilaya Kasakazi ‘A’ Mkoa wa
Kaskazini Unguja.
Kwa mujibu wa maelezo ya serikali
yaliyosomwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed
Aboud Mohamed kwa waombolezaji,marehemu Hamid Ameir alishiriki
kikamilifu katika Mapinduzi yaliyowakomboa wananchi wa Zanzibar kutoka
kwa wakoloni mwaka 1964.
Marehemu ambaye alizaliwa 01
Januari, 1928 alijiunga na Chama cha Afro Shirazi mwaka 1957 na
kushiriki kuunda Umoja wa Vijana wa chama hicho (ASPYL).
Marehemu Hamid Ameir alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali na Chama cha Afro Shirazi na baadae Chama cha Mapinduzi.
Aliwahi kuwa kamanda wa Jeshi la Ukombozi na pia kushika nafasi ya naibu Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Viongozi wengine wa kitaifa
walioshiriki mazishi ya mwasisi huyo wa Mapinduzi ni pamoja na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Makamu wa Rais Mstaafu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal pamoja na
mawaziri, makatibu wakuu na viongozi wa dini.
Kutokana na kushiriki kwake
katika Mapinduzi na kwa mchango wake katika kulinda na kuendeleza
Mapinduzi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
alimtunuku mzee Hamid Ameir Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya
Mapinduzi katika sherehe zilizofanyika tarehe 11 Janauri, 2014 katika
Viwanja vya Ikulu, Zanzibar.
Mwaka huo huo, tarehe 25 April,
2014 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
alimtunuku mzee Hamid Ameir, Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya
Muungano.
Tags
HABARI KITAIFA