“Serikali hii haina utumishi kwa
mtu aliyeharibu kazi. Usije ukaharbu hapa Itilima ukadhani utaenda Bunda
kuendelea na kazi. Serikali ya awamu hii haina nafasi na watumishi wa
aina hiyo,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo
(Ijumaa, Machi 4, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya
Itilima kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambao ameuzindua leo
hii wilayani Itilima, mkoani Simiyu.
“Watumishi wenzangu huu ni wakati
wa kubadilika na kuona mwelekeo wa Serikali hii ya awamu ya tano ukoje.
Jukumu letu ni kuwatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi zao,
rangi wala dini zao,” alisisitiza.
Waziri Mkuu aliwahakikishia
watumishi hao kwamba Serikali inatambua changamoto walizonazo kutokana
na upya wa wilaya hiyo na mkoa huo na akawaahidi kuwa itaboresha
mazingira yenu. “Msiwaadhibu wananchi kwa kisingizio cha mazingira
magumu ya kazi zenu, tunajua mnayo madai ya nauli, posho za mafunzo,
kupandishwa madaraja na malimbikizo ya likizo,” alisema huku
akishangiliwa.
Alisema Serikali itayalipa madeni
hayo japo haitamaliza yote kwa wakati mmoja ila ana uhakika wa
kukamilisha walau kwa asilimia 80.
Mapema, akitoa taarifa ya wilaya
hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Bibi Georgina Bundala alisema wilaya hiyo
iliyoanzishwa Machi 2012 na kupata Halmashauri Julai 2013 haina kituo
cha polisi cha wilaya, haina gereza, Ofisi za TAKUKURU, mahakama ya
wilaya wala benki.
Alisema wilaya hiyo haina
hospitali ya wilaya ila akabainisha kuwa wamekwishatenga eneo la ekari
30 kwa ajili ya ujenzi huo. “Pia tumekwishapima viwanja 123 na eneo la
kujenga taasisi lenye ekari 143.8 limefanyiwa uthamini na fidia
kukamilika,” alisema.
Tags
HABARI KITAIFA