Dar es Salaam.
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi
Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Mkoa wa
Kilimanjaro kuwafikisha mahakamani madereva wote na makondakta
wanaowatoza abiria nauli kubwa tofauti na zilizopangwa na ofisi hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Afisa
Mfawidhi Bw.Tadei Mwita alipokuwa akijibu kero ya mkazi wa mkoa huo kwa
njia ya simu iliyotolewa na Gazeti la Mwananchi Machi 04, mwaka
huu,iliyozungumzia daladala zinazofanya safari zake kati ya Moshi Mjini
– Himo kuwatoza nauli ya shillingi 1000 abiria wanaoshuka maeneo ya
Kiboriloni, Sango Pumuani na Kawawa road tofauti na nauli iliyopangwa na
SUMATRA katika vituo hivyo.
“Kuanzia wiki ijayo wadau wote
watakao kuja kuomba leseni kwa ajili ya usafirishaji wa abiria ndani ya
mkoa huu watahitajika kuonyesha nauli watakazo toza abiria katika vituo
vya katikati kabla ya kufika kituo cha mwisho cha safari zao,”alisema
Bw.Mwita.
Bw.Mwita alisema hivi sasa
SUMATRA Mkoa wa Kilimanjaro imeanzisha utaratibu wa kuwataka wadau wote
wanaotarajia kuanza kutoa huduma za usafiri wa daladala mkoani hapo
kuonyesha nauli watakazo toza katika vituo vya katikati kabla ya kufika
kituo cha mwisho.
Hata hivyo Afisa huyo
aliwashauri wakazi wa maeneo kama kiboriloni kwa sasa kupanda daladala
za Kiboriloni kwa kuwa zipo nyingi ili kuepuka usumbufu unaojitokeza.
Tags
HABARI KITAIFA