JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO
YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI
TANZANIA
TAARIFA YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA
HABARI TAREHE 11.03.2016
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
limefanya Operesheni na Msako mkali katika Wilaya zake zote na kukamata makosa
mbalimbali. Operesheni hiyo ilianza kufanyika tarehe 22/02/2016 hadi
06/03/2016.
![]() |
Katika Operesheni hiyo jumla ya silaha
haramu 19 aina ya Gobore zimesalimishwa
na silaha saba (7) zimekamatwa za
watu waliokaidi utii wa sheria, mitambo miwili ya kutengeneze silaha hizo haramu
imekamatwa pamoja na watuhumiwa saba ambao ni:-
![]() |
| Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Lazoro Mambosasa akionyesha Magobole hayo kwa waandishi wa habari PICHA ZOTE NA BANDA BLOG |
1.
KHAMISI MTANDIKA, mwenye miaka 40, mkuliama alikamatwa
akiwa na silaha moja aina ya gobore, mideki mtatu ya kusafishia silaha, baruti
gramu 12 na goroli.
2.
MAJUTO MAGANA, mwenye miaka 31, mkulima alikamatwa na
gobore moja.
3.
JAVAN WILLIAM, mwenye miaka 36, mkulima alikamatwa na
gobore moja.
4.
COSMAS MASWAGA, mwenye miaka 55, mkuliama alikamatwa na
gobore moja na mtambo mmoja wa kutengenezea silaha.
5.
MBARAKA KITINDI, mwenye miaka 45, mkulima alikamatwa na
gobore moja na mtambo mmoja wa kutengenezea silaha.
6.
COSMAS EZEKIEL MKENZA, mwenye miaka 34, mkulima alikamatwa
na gobore moja.
7.
SANYA MZOGOLE, mwenye miaka 45, mkulima alikamatwa na gobore
moja.
Watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha MANDA Tarafa ya MPWAYUNGU
Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma na
wamekuwa wakimiliki silaha hizo kinyume cha sheria na wakizitumia katika uhalifu mbalimbali hasa
uwindaji haramu katika hifadhi ya RUAHA inayopakana na mkoa wa Iringa. Kutokana
na operesheni hiyo watu 19 waliweza kusalimisha silaha zao katika ofisi za
serikali za vijiji na hawakuchukuliwa hatua kwa kuwa walitii sheria bila
shuruti.
Katika Wilaya za Dodoma, Kondoa na
Kongwa walikamatwa watuhumiwa 32 wa makosa ya Kupatikana na Bhangi, jumla ya
misokoto misokoto 672 ilikamatwa.
Watuhumiwa 11 walikamatwa kwa kosa la Kupatina na Pombe haramu ya Moshi
na jumla ya lita 260 zilikamatwa. Watuhumiwa
7 walikamatwa kwa kosa la Kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Mirungi
Kilogram 43.
Pia Operesheni ilihusisha makosa ya
Usalama barabarani na kukamatwa kwa jumla ya pikipiki 265 kwa makosa mbalimbali,
ambapo pikipiki 241 zilitozwa faini na kiasi cha fedha Tsh. 7,230,000/=
zilipatikana kutokana na tozo.
Napenda kutoa wito kuwa, Msako mkali
unaendelea na watu wote wanaomiliki silaha haramu kinyume cha Sheria
wasalimishe silaha hizo kwa hiari kwenye
Ofisi za Serikali na vituo vya Polisi mapema iwezekanavyo na
hawatachukuliwa hatua. Wale wote
wanaomiliki silaha kinyume cha Sheria wasiotayari kusalimisha wafichuliwe ili
wachukuliwe hatua za kisheria dhidi ya umiliki haramu wa silaha. Aidha wananchi
waache kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa aina yoyote na kufanya kazi halali
kujipatia kipato halali kwa familia zao kwani msako utakuwa endelevu wasije
wakaishia jela na kuziacha familia zao zikiteseka.
Imetolea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP- LAZARO BENEDICT
MAMBOSASA.
Tags
HABARI KITAIFA




