Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege mara baada
kwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati alipopitaka mkoani humo
akielekea Nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko, hii
ni mara ya kwanza kwenda kupumzika kijijini kwake toka alipchaguliwa na
kauapishwa kushika madaraka ya kuongoza Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
mwezi Oktoba mwaka jana.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John
Mongela amemshukuru Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya
kuamuru kufunguliwa kwa barabara inayopita kandokando ya uwanja wa ndege
kuelekea Kayenze iliyokuwa imefungwa kwa miezi miwili na kuleta adha
kubwa kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo.
Mara baada ya Rais Magufuli
kuamuru barabara hiyo ifunguliwe mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela
pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza Uongozi mzima wa
mkoa huo waliongozana kwenda Kayenze na kuwatangazia wananchi kwamba
wako huru kutumia barabara hiyo kwakuwa Mh. Rais ameamuru ifunguliwa na
sisi tumekuja kutekeleza agizo la rais na sasa barabara hii
imefunguliwa.
(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWE-MWANZA)
Mke wa Rais Mama Janet Magufuli
akishuka kwenye ndege wakati Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli
alipowasili uwanjani hapo akielekea Chato Mkoani Geita kwa mapumziko.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza
Mh. John Mongela mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mwanza
leo.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana Mkuu wa wilaya ya
Nyamagana Mh. Baraka Konisaga kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza leo.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa kamati ya
Amani mkoani Mwanza wakati alipowasili uwanjani hapo akielekea Chato.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mh.Altaf Mansour
mlezi wa shirikisho la Vyuo vikuu CCM Kanda ya Ziwa, Kushoto ni Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mh.Altaf Mansour
mlezi wa shirikisho la Vyuo vikuu CCM Kanda ya Ziwa, Kushoto ni Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana wana CCM waliofika
uwanjani hapo kumpokea, Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John
Mongela.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipigiwa saluti na mmoja wa wakuu wa
vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza waliofika uwanjani hapo
kumpokea.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana afisa habari wa ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw. Atley Kuni .
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akielekea kukagua vikundi vya ngoma na kwaya.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na Mkewe mama Janet Magufuli
wakiangalia vikundi vya ngoma wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege
wa Mwanza leo wakielekea Chato kwa mapumziko.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janet Magufuli
wakiwapungia wachenza goma wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa Ndege wa
Mwanza.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na askari wa kikozi cha Zimamoto uwanjani hapo.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiangalia kwaya ya AIC Makongoro
ambayo iliimba wimbo wa kuhamasisha kuitunza amani ya nchi na
kumhamasisha kiasi cha kumfanya kujumuika nao na kuimba pamoja na
wanakwaya hao.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na wanakwaya wa AIC
Makongoro ya jijini Mwanza wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa
Mwanza.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na wanakwaya wa AIC
Makongoro ya jijini Mwanza wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa
Mwanza.
Wadau Issa Michuzi kulia na Pius Lugonzibwa kushoto walikuwepo katika mapokezi hayo.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akwapungia mkono wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Mwanza.
Rais wa jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya wananchi
waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa mwanza katikati ni Mkuu wa
mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Nyamagana Mh. Baraka Konisaga.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John
Mongela akimshukuru Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya
kuamuru kufunguliwa kwa barabara inayopitka kandokando ya uwanja wa
ndege kuelekea Kayenze.
Mh.Altaf Mansour mlezi wa
shirikisho la Vyuo vikuu CCM Kanda ya Ziwa alikuwepo katika mapokezi
hayo , Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga.
Baadhi ya wanahabari waliokuwepo
uwanjani hapo wakifurahia kwa kugonganisha chupa za soda kinywaji
ambacho Mh. Rais Dk John Pombe Magufuli alitoa ofa kwa wananchi wote
waliokuwepo uwanjani hapo, kulia ni Shila Kutoka ITV Mwanza na kushoto
ni Atley Kuti afisa habari wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli
akiondoka kwenye kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza mara baada kupata
kifungua kinywa kwenye mgahawa wa Victoria Catering.
Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli
akipiga picha ya pamoja na kwaya ya AIC Makongoro na baadhi ya viongozi
wa mkoa wa Mwanza kabla ya kuelekea Chato mkoani Geita.
Tags
HABARI KITAIFA