……………………………………………………………………………………
Huduma ya usafiri wa reli ya Kati
iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi miwili sasa imerejea kufuatia
kukamilika kwa ukarabati wa reli hiyo katika eneo la kidete wilayani
kilosa, mkoani Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo baada ya kukagua na
kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo ya Magulu, Munisagara,
Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.
“Hakikisheni mnailinda reli hii
kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko vizuri na treni ya kwanza
kutoka Dar Es Salam kwenda bara itapita na kumaliza changamoto ya
usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wanaotumiia reli hii”.Amesema
Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amewataka wananchi
wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara, Mzaganza, Kidete, Godegodena
Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na mafuriko ya mto Mkondoa kuacha
Kilimo cha kuelekeza Maji kwenye reli bali washirikiane na Serikali
kudhibiti maji hayo kwenda kwenye hifadhi ya reli.
AmesemaShirika la Reli Tanzania
(TRL) linaendeleakuhakikisha kuwa treni inayopita kwenye reli ya Kati
inapata mzigo mwingi wa kusafirisha kutoka bandarini za Tanga naDar Es
Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mpanda, hivyo wafanyabiashara
watumie fursa hiyo ili kupunguza mzigo unaosafirishwa kwa Nadia ya
barabara.
Waziri Profesa Mbarawa
ameteembelea bwawa la Kidete linaloelezwa kuwa chanzo cha mafuriko pindi
linapojaa wakati wa mvua za Vuli na Masika katika mikoa ya Dodoma na
Iringa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa John
Henjewele amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa ofisi yake
itafuatilia kwa karibu malalamiko ya wananchi wanaoishi karibu na reli
ya Kati ili kuyapatia ufumbuzi na kuwataka wananchi hao kuitumia fursa
ya kuwa karibu na reli kunufaika kiuchumi.
Takribani Shilingi millions 926
zimetumika katika ukarabati wa reli hiyo kufuatia uharibifu uliotokea
mwezi Januari na kukata Mawasiliano ya reli Kati ya mikoa ya Dodoma na
Morogoro na kusababisha Safari za treni kutoka bara kuishia Dodoma.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,, Uchukuzi na Mawasiliano Serikalini.
Tags
HABARI KITAIFA