Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es Salaam
(Dawasco ) Mhandisi Cyprian Luhemeja akishiriki zoezi la usafi katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili na watumishi wa Dawasco.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akiweka maji katika
moja ya mashine inayotumika kuzibulia miundombinu ya maji taka
ijulikanayo kama Jet Machine.
Wafanyakazi
wa Dawasco wakijaribu kuweka sawa mpira wa kunyunyiza maji ili kuondoa
vumbi wakati wakifanya usafi katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Wafanyakazi wa Dawasco wakiendelea na usafi katika maeneo mbalimbali ya Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.
Afisa
Mtendaji Mkuu Dawasco Mhandisi Cyprin Luhemeja akimueleza jambo Mkuu wa
Wilaya ya Ilala,Raymond Mushi baada ya kumaliza kufanya usafi katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Wengine ni wafanyakazi wa Dawasco.
Wafanyakazi wa Dawasco wakiwa na vifaa vya kufanyia usafi.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi ,Cyprian Luhemeja akitoa msaada wa
vitu mbalimbali kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala ,Raymond Mushi ambaye pia
alikabidhi kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbi.
Baadhi
ya vitu vilivyotolewa na Dawasco mara baada ya wafanyakazi wake
kumaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala,Raymond Mushi akizungumza na wafanyakazi wa Dawasco
mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika Hospitali hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Dawasco akizungumza na wanahabri mara baada ya kufanya
zoezi la usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Meneja
wa Dawasco eneo la Magomeni Mhandisi Paschal Fumbuka akizungumza na
wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika Hospitai ya
Taifa ya Muhimbili.
Baadhi ya vitendea kazi vya Dawasco vikiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi.
Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .
………………………………………………………………………………………………………..
Neema Mwangomo, Afisa Uhusiano, MNH.
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO)
limefanya usafi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la
kudumisha ushirikiano, lakini pia kutekeleza agizo la Rais Dk John
Magufuli la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini.
Usafi huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi , Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga wa Muhimbili, Agnes Mtawa
pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja .
Usafi huo umefanyika katika maeneo yote muhimu ya Hospitali ikiwemo utoaji wa maji taka .
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Mkuu wa wilaya ya
Ilala Raymond Mushi amesema zoezi la kufanya usafi lazima halina budi
kuwa endelevu ili kuhakikisha maeneo yote yanakua safi lakini pia epuka
magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtawa amewashukuru DAWASCO kwa
uamuzi wa kuja kufanya usafi MNH ambapo ametumia fursa hiyo pia
kuwaomba wafanyakazi wa Shirika hilo kujitolea kuchangia damu ili kuokoa
maisha ya wagonjwa ambao wanahitaji damu.
Pamoja na mambo mengine DAWASCO wametoa msaada wa vitu
mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa ambao wamelazwa Hospitalini hapo ambao
wanapatiwa matibabu .
Tags
MAZINGIRA








