Kikosi cha awamuya kwanza cha wachezaji 26 cha timu taifa ya England kimetangazwa asubuhi ya leo na kocha Roy Hodgson.
Kufuatiwa kumalizika kwa ligi kuu ya England, Three Lions wataanza maandalizi ya michuano hiyo ambapo wamepangwa kwenye kundi linalohusisha timu za Russia, Wales na Slovakia katika kundi B.
Katika kikosi hicho kilichotangazwa leo mshambuliaji wa Manchester United, mwenye umri wa miaka 18, Marcus Rashford amejumuishwa.
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere pia amejumuishwa pamoja na kucheza mechi 3 tu kwenye premier league msimu huu baada ya kuwa nje kwa majeruhi kwa muda mrefu.
Kiungo wa Manchester City Fabian Delph nae amepata nafasi pamoja na kuanza jumla ya mechi 8 tu tangu alipojiunga na City akitokea Aston Villa.
Winga wa Newcastle Andros Townsend nae amefanikiwa kuitwa kikosini kuungana na wachezaji wenzake wa zamani Dele Alli na Eric Dier, wakati Theo Walcott akitemwa.
Mfungaji bora wa Premier League Harry Kane anaunda safu ya ushambuliaji na staa wa Leicester City Jamie Vardy, Wayne Rooney, Daniel Sturridge, pamoja na Rashford.
Danny Drinkwater ni mchezaji mwingine kutoka kwa mabingwa wa EPL kuwemo ndani ya kikosi.
Wachezaji wengi wataanza kukutana katika kambi iliyopo St. GEORGE Park kuanzia jumatano. England watakutana na Uturuki kwenye mchezo wa kirafiki mnamo May 22, kabla ya kukutana na Australia mnamo Mei 29 na kisha Portugal wataenda Wembley tarehe 2 June.
Hodgson Atatangaza kikodi cha wachezaji 23 kwa ajili ya Euro mapema June kabla ya kuelekea Ufaransa.
GOALKEEPERS: Joe Hart, Fraser Forster, Tom Heaton
DEFENDERS: Ryan Bertrand, Gary Cahill, Nathaniel Clyne, Danny Rose, Kyle Walker, Chris Smalling, John Stones
MIDFIELDERS: Dele Alli, Ross Barkley, Fabian Delph, Eric Dier, Danny Drinkwater, Jordan Henderson, Adam Lallana, James Milner, Raheem Sterling, Andros Townsend, Jack Wilshere
STRIKERS: Harry Kane, Marcus Rashford, Wayne Rooney, Daniel Sturridge, Jamie Vardy
Tags
MICHEZO KIMATAIFA